Loading...

Mchezaji afukuzwa kazi kisa wizi wa simu


Klabu ya ligi ya daraja la kwanza nchini Ufaransa Nice imemfuta kazi mchezaji wake Lamine Diaby - Fadiga baada ya kukiri kuiba saa ilio na thamani ya £62,000 kutoka kwa mchezaji mwenzake Kasper Dolberg.

Mshambuliaji wa Denmark Dolberg, 21, aliibiwa saa yake katika chumba cha maandalizi mnamo tarehe 16 mwezi Septemba na kuripoti kisa hicho kwa maafisa wa polisi.

Mshambuliaji Fadiga mwenye umri wa miaka 18 ameiwakilisha Ufaransa katika kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18.

''Nice na Lamine Diaby - Fadiga waliwachana siku ya Jumanne'' , ilisema taarifa ya klabu hiyo.

''Kufuatia wizi huo wa saa ya Kasper Dolberg kutoka katika chumba cha maandilizi na kukiri kwa mchezahi huyo , klabu hiyo iliamua kufutilia mbali kandarasi yake mara moja''.

Mbali na maswala ya kifedha na michezo . Klabu ya Nice haiwezi na haitakubali tabia kama hiyo ambayo ni kinyume na lengo la kuwaungunisha wafanya kazi wote wa klabu hiyo na wanachama wote wa Rouge et Noir .

Dolberg alijiunga na Nice kutoka klabu ya Ajax msimu huu, huku Diaby - Fadiga akiwa katika klabu hiyo kwa muda wa miaka mitatu.

Nice ipo katika nafasi ya sita katika ligi hiyo, inacheza ugenini dhidi ya klabu ilio katika nafasi ya tatu Nantes siku ya Jumamosi.
Mchezaji afukuzwa kazi kisa wizi wa simu Mchezaji afukuzwa kazi kisa wizi wa simu Reviewed by Zero Degree on 10/02/2019 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.