Mourinho mbioni kujiunga na klabu hii ya Bundesliga
Jose Mourinho anahusishwa kukabidhiwa klabu ya Borussia Dortmund kama meneja mpya huku ikidawa timu hiyo tayari imeshaanza mazungumzo ya awali na kocha huyo wa zamani wa Manchester United.
Mourinho yupo tayari kurudi kwenye majukumu ya kocha huku akionekana kuvutiwa zaidi na Dortmund ambayo ipo kwenye michuano ya Champions League ikiwa na wachezaji nyota kama Jadon Sancho, Marco Reus na Paco Alcacer.
Kwa kipindi kirefu sasa, Mourinho amekuwa hana timu tangu alivyo timuliwa Manchester United mwaka jana, hata hivyo tayari ameshajifunza kuzungumza lugha ya Kijerumani kwa mujibu wa gazeti la Bild.
Gazeti hilo la michezo kutoka nchini Ujerumani, Bild limeripoti kuwa, Mourinho ndiyo chaguo namba moja (1) kwa klabu ya Dortmund ambaye atachukua mikoba ya Lucien Favre, anayeonekana kusuasua kwenye ligi ya Bundesliga mbele ya vigogo Bayern.
Mourinho tayari ameshakuwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa klabu ya Dortmund, Hans-Joachim Watzke.
Hata hivyo usiku wa leo, Borussia Dortmund itakuwa ugenini Italia kukabiliana na miamba ya nchi hiyo Inter Milan kwenye michuano ya UEFA Champions League.
Mchezo wa ‘group’ F, ambapo inaongoza kwa pointi 4 ikifatiwa na Barcelona wenye alama 4, Slavia Praha wakiwa na ponti 1 na Inter Milan wakiburuza mkia kwa alama 1.
Mourinho tayari ameshakuwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa klabu ya Dortmund, Hans-Joachim Watzke.
Hata hivyo usiku wa leo, Borussia Dortmund itakuwa ugenini Italia kukabiliana na miamba ya nchi hiyo Inter Milan kwenye michuano ya UEFA Champions League.
Mchezo wa ‘group’ F, ambapo inaongoza kwa pointi 4 ikifatiwa na Barcelona wenye alama 4, Slavia Praha wakiwa na ponti 1 na Inter Milan wakiburuza mkia kwa alama 1.
Mourinho mbioni kujiunga na klabu hii ya Bundesliga
Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2019 08:25:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2019 08:25:00 AM
Rating: