Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Februari 13, 2019


Chelsea wanata kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuchukua nafasi ya Sarri ambaye amekuwa akisuasua.

Beki wa kulia wa Crystal Palace Muingereza Aaron Wan-Bissaka anatakia na klabu ya Borussia Dortmund. Mchezaji huyo mwenye miaka 21 pia anatakiwa na Manchester City. (Sun)

Real Madrid wanaamini wakati mgumu anaopitia kocha wa Chelsea Maurizio Sarri utawarahisishia kumsajili kiungo Mbelgiji Eden Hazard, 28, mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Golikipa wa Paris St-Germain Gianluigi Buffon, 41, amesema kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya msimu huu itakuwa ni namna bora kwake yeye kustaafu kucheza mpiara.

Kiungo Mjerumani wa Arsenal Mesut Ozil amekuwa akipigiwa chapuo katika vilabu vingine na wawakilishi wake, huku mustakabali wake dimbani Emirates ukibaki kuwa wa mashaka. (Telegraph)

Real Madrid wataminyana na Barcelona kumsajili straika wa Benfica Luka Jovic, 21, kwa kutangaza dau la euro milioni 45 kwa nyota huyo anayechezea kwa mkopo klabu ya Eintracht Frankfurt. (Bild)

Wawakilishi wa mchezaji wa Everton raia wa Brazil Richarlison, 21, wamefanya mazungumzo na hav Atletico Madrid kuhusu mshambuliaji huyo kuhamia vigogo hivyo vya Uhispania. (AS)

Tottenham inataraji kumsajili winga wa Inter Milan na timu ya taifa ya Croatia Ivan Perisic, 30, ambaye alikuwa aknyemelewa na Arsenal mwezi Januari. (Tuttosport, kupitia Football Italia)

Mchezaji wa zamani wa Manchester United raia wa Ureno Luis Nani, 32, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Sporting CP, ananyemelewa na klabu ya Ligi ya Marekani MLS side Orlando City.


Winga raia wa Wales Gareth Bale, 29, anaongea kwa ishara tu na wachezaji wenzake wa Real Madrid kwa kuwa bado hajajifunza Kihispania, amesema mchezaji mwenzake Marcelo. (Marca)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Februari 13, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Februari 13, 2019 Reviewed by Zero Degree on 2/13/2019 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.