Loading...

Tanzia: Msanii Godzilla afariki dunia


Tasnia ya Bongo Fleva imepata pigo baada kuondokewa na Rapa maarufu nchini, Golden Mbunda ‘Godzilla‘ ambaye amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo Jumatano, Februari 13, 2019 akiwa nyumbani kwao, maeneo ya Mbezi Salasala, Dar es Salaam.

Mtu wake wa karibu ameeleza kuwa presha ilishuka na sukari ilipanda pamoja na kuumwa na tumbo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Godzilla amefariki dunia ghafla nyumbani kwao Salasala jijiji Dar es Salaam. Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

Kwa mujibu wa Wauguzi wa Hospital ya Lugalo, wamesema Godzilla aliletwa hapo akiwa ameshafariki, hivyo wamehifadhi mwili tu.
Tanzia: Msanii Godzilla afariki dunia Tanzia: Msanii Godzilla afariki dunia Reviewed by Zero Degree on 2/13/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.