Loading...

Msajili atoa siku 7 kwa Chadema


Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania ameandika barua kwenda kwa chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema akikitaka kutoa maelezo kwa nini kisichukuliwe hatua kwa kutokufanya uchaguzi wa viongozi wake.

Barua ya Msajili iliyoandikwa Oktoba 1, 2019 na kusainiwa na Sisty Nyahonza kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa inasema uongozi wa Chadema chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe umemaliza muda wake tangu Septemba 14, 2019.

Katika barua hiyo, msajili amekitaka chama hicho kutoa maelezo hayo kabla ya Oktoba 7, 2019 saa 9:30 mchana.

“Chadema mnapaswa kuwasilisha maelezo kwa msajili wa vyama vya siasa kwa nini msichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya vyama vya siasa, katiba na kanuni zenu.”

“Maelezo yenu yawasilishwe ofisi ya msajili wa vyama vya siasa sio zaidi ya Oktoba 7, 2019 saa 9:30 mchana,” anasomeka barua hiyo

Katika maelezo ya msajili anakitaka chama hicho kuheshimu sheria za nchi hususan sheria ya vyama vya siasa, katiba na kanuni za Chadema katika menejimenti ya chama.
Msajili atoa siku 7 kwa Chadema Msajili atoa siku 7 kwa Chadema Reviewed by Zero Degree on 10/03/2019 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.