Loading...

Mwana FA, Dude wafika kilele cha mlima Kilimanjaro


MWIGIZAJI mkongwe Kulwa Kikumba ‘Dude’ na msanii wa Hip hop nchini, Hamis Mwinjuma ‘Mwana Fa’, wamefika kilele cha Uhuru cha mlima Kilimanjaro umbali wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari kupitia kampeni ya Twenzetu Kileleni iliyoanza wiki iliyopita.

Mastaa kibao walishiriki katika kampeni hiyo ya kuhamaisha utalii wa ndani lakini wengi wao walishindwa kumudu kufika katika kilele cha Uhuru na wakaishia kwenye vituo vya mwanzoni kwa sababu mbalimbali.

Kwa hatua hiyo, Dude anakuwa msanii wa kwanza wa filamu Bongoi kufika kwenye kilele hicho huku Mwana Fa akiwa msanii wa pili wa Bongo Fleva baada ya Lady Jay Dee aliyewahi kufika kwenye kilele cha Uhuru mwaka 2013.
Mwana FA, Dude wafika kilele cha mlima Kilimanjaro Mwana FA, Dude wafika kilele cha mlima Kilimanjaro Reviewed by Zero Degree on 10/04/2019 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.