Loading...

NEMC yakamata shehena ya mifuko ya plastiki


Polisi kwa kushirikiana na maofisa wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), wamekamata shehena ya mifuko ya plastiki bando 53 zenye mifuko 6,360. Mifuko hiyo ilikamatwa Oktoba 18 na mtu mmoja anashikiliwa na polisi.

Mwanasheria wa Nemc, Manchare Heche alisema wamesikitishwa na kitendo cha uwapo wa mifuko hiyo iliyopigwa marufuku nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwananchi, Heche alisema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa hakikubaliki huku akitumia nafasi kutoa wito kwa Watanzania kuacha kutengeneza na kutumia, kuuza au kusambaza mifuko ya plastiki.

Naye kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandari, Benedict Mapujila alisema mifuko hiyo ilikamatwa juzi saa 3:00 usiku eneo hilo wakati mtuhumiwa akijaanda kuipeleka Zanzibar.

“Alikuwa anataka kuisafirisha kwa njia ya meli, lakini kabla ya kufanikiwa kwenda alikamatwa wakati wa ukaguzi. Bado tunaendelea na upelelezi atuonyeshe alipata wapi hii mifuko wakati ilishapigwa marufuku.
“Wananchi na Watanzania tuheshimu sheria zilizopo, Serikaliu ilishapiga marufuku matumizi, lazima tutii kutoitumia. Madhara ya mifuko hii yalishasemwa,” alisema Kamanda Mapujila.
NEMC yakamata shehena ya mifuko ya plastiki NEMC yakamata shehena ya mifuko ya plastiki Reviewed by Zero Degree on 10/21/2019 09:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.