“Siendi kokote, hapa ni nyumbani” - Ozil
“Unaweza ukapitia wakati mgumu, kama hivi, lakini hicho sio kigezo cha kukimbia na mimi sitafanya hivyo,” Ozil alimwambia Ornstein. “Niko hapa hadi walau mwaka 2021.”
“Nilisema kwamba Arsene Wenger alikuwa sababu kubwa sana kwa mimi kujiunga na Arsenal — na alikuwa hakika — lakini hatimaye nilisani mkataba na klabu hii,” Ozil aliendelea kusema. “Hata wakati Arsene alipotangaza kuwa anaondoka, nilitaka kubakia kwa sababu napenda kuichezea Arsenal na hiyo ni sababu ya mimi kuwa hapa kwa miaka sita.
“Wakati nilipoondoka Real Madrid, hakika ilikuwa ni wakati mgumu kwa Arsenal. Lakini niliamini katika uwezo wetu na kwa umoja tulifanikiwa. Hivi kairibuni mambo yamekuwa magumu na kuna mabadiliko makubwa. Lakini najivunia kuwa mchezaji wa Arsenal, mshabiki na ninafurahia kuwa hapa. Kila mara watu wanionapo mitaani huwa nasema, ‘Hapa ni nyumbani’. Siendi kokote.”
“Ninayajua yote yaliyokwisha semwa,” Ozil anaongeza kuhusiana na kwanini hachezeshwi. “Inakatisha tamaa, bila shaka. Lakini kama mchezaji wa kimataifa, ni lazima niheshimu uamuzi wa kocha. Kutojumuishwa, kutazama michuano nikiwa nyumbani, kuna nifanya nijihisi kukosa msaada.
“Nataka kuwa mmoja wao, nataka kuiunga mkono wenzangu kufanikiwa. Sifanyi mazoezi kila mara kwa ajili hiyo, niko tayari kucheza. Hii haitakiwi kuhusishwa na kocha au mimi, bali klabu tu. Lazima nijito kwa kila kitu, niwe imara na mwenye matazamio, na ninafanya mazoezi ya nguvu ili kuwa tayari.
“Michezo ya kabla ya msimu ilienda vizuri na ingawa mambo yaliingiliwa na shambulizi, kuanzia hapo nimekuwepo tu na wakati kocha aliponijumuisha nimekuwa nikiwa tayari, nilicheza na mara zote nimejitahidi kujitoa katika kiwango cha juu zaidi.
“Nimefanya mazoezi katika kiwango kile kile maisha yangu yote lakini kwa sababu ya kukosa nafasi hivi karibuni, ninafanya kazi ya ziada na kocha wa mazoezi ya viungo ndani ya 'gym' ili kuwa imara zaidi kupita kawaida. Ninajua kinachohitajika na ninajiamini.”
“Siendi kokote, hapa ni nyumbani” - Ozil
Reviewed by Zero Degree
on
10/18/2019 12:05:00 PM
Rating: