Wanafunzi 39 wanusurika kufa kwa radi mkoani Geita
Taarifa iliyotolewa jana Ijumaa Oktoba 18, 2019 na mganga mkuu wa mkoa wa Geita, Josephat Simeo inaeleza kuwa wanafunzi 24 wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Nzera na 15 wamepatiwa matibabu katika zahanati ya Nkome.
Dk Simeo amesema radi hiyo imesababisha watoto kupata mshtuko na kuzimia lakini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza wanaendelea vizuri na tayari wanafunzi 36 wameruhusiwa kutoka hospitali.
Wanafunzi 39 wanusurika kufa kwa radi mkoani Geita
Reviewed by Zero Degree
on
10/19/2019 07:05:00 AM
Rating: