Uturuki kuendeleza mashambulizi Syria
Amesema hayo wakati pia akithibitisha kwamba wanamgambo hao wameshaanza kuondoka kutoka kwenye eneo hilo la kaskazini mwa Syria. Makubaliano ya kusitisha makabiliano yalifikiwa kati ya Uturuki na Marekani jana.
Hata hivyo mapema leo shirika la habari la AP wanaharakati wa haki za binaadamu na shirika linalofuatilia mzozo huo wa Syria wameripoti mapema hii leo kuendelea kwa mapigano katika mji wa Ras al Ayn licha ya makubaliano hayo madai ambayo Erdogan ameyapuuzilia mbali.
Aidha Erdogan amesema wiki ijayo atakutana na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin na kufanya mazungumzo ya kina kuhusu eneo hilo kwa lengo la kuleta amani.
Uturuki kuendeleza mashambulizi Syria
Reviewed by Zero Degree
on
10/19/2019 07:15:00 AM
Rating: