Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Oktoba 11, 2019


Kocha wa Juventus Maurizio Sarri anataka kumsajili beki wa kushoto Mtaliano Emerson, 25, kutoka Chelsea. (Express)

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa klabu ya Rostov na raia wa Norway Mathias Normann, 23, mwezi Januari.

Jose Mourinho amekataa ofa ya kuifundisha klabu ya Lyon kwa kuwa ameshapata klabu nyengine, hayo ni kwa mujibu wa rais wa ligi ya Ufaransa, Jean-Michel Aulas. (Goal)

Manchester United inajipanga kulipa kitita cha pauni milioni 130 kuwanyakua wachezaji wawili wa Leicester na England; mlinzi Ben Chilwell na kiungo James Maddison, wote wana miaka 22. (Sun)

Arsenal wanamfuatilia kwa karibu kiungo kinda wa klabu ya Feyenoord ya Uholanzi Orkun Kokcu,18, mwenye thamani ya pauni milioni 20.

Hata hivyo kuna ripoti zinadai kuwa klabu ya Chelsea kwa sasa ndio wanapigiwa upatu zaidi kumnasa beki wa kushoto Chilwell pale marufuku dhidi yao ya usajili itakapokwisha. (Mail)

Man United inataka kusajili wachezaji wapya 8 katika kipindi cha misimu miwili ijayo na tayari wameshaandaa orodha ya wachezaji hao. (Telegraph)

Christian Eriksen, 27

Real Madrid hawataki kupoteza bahati kwa kutomsajili kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, mpaka mwisho wa msimu ambapo kuna uwezekano akaongeza mkataba na klabu yake ya Tottenham. (Marca)

Tottenham wana matumaini kuwa watamuuza Eriksen mwezi Januari tili kuzuia wasimpoteze bure mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake utakuwa unaisha.

Manchester City wanatafakari juu ya kufanya usajili wa mwezi Januari kwa kumnunua beki wa timu ya Benfica Ruben Dias, 22, ambaye pia anahusishwa na uhamishi kuelekea Manchester United. (Mirror)

Japo rais wa Real Madrid Florentino Perez anataka kumsajili Eriksen, kipaumbele cha kocha Zinedine Zidane bado ni kiungo wa Manchester United Paul Pogba, 26.

Beki wa Barcelona Gerard Pique, 32, alikaribia kuinunua klabu ya Notts County mwishoni mwa msimu uliopita. (ESPN)

Arsenal wapo katika mazungumzo na klabu ya Uturuki Fenerbahce juu ya usajili wa mkopo wa kiungo Mesut Ozil, 30. (Takvim)

Kocha wa Everton Marco Silva amepewa michezo mitatu ya kubadili hali ya mambo ama atimuliwe kazi. (Star)

Claudio Ranieri

Sampdoria wanakaribia kumteua kocha wa zamani wa Leicester Claudio Ranieri, 67, kama kocha wao mpya. (Tuttosport)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Oktoba 11, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Oktoba 11, 2019 Reviewed by Zero Degree on 10/11/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.