Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Oktoba 3, 2019


Aliyekuwa kocha wa klabu ya Chelsea Maurizio Sarri ana matumaini ya kuungana tena na kiungo mkabaji N'Golo Kante, 28. Sarri ambaye kwa sasa anainoa Juventus yupo tayari kumnunua kiungo huyo raia wa Ufaransa kwa kitita cha takribani pauni milioni 70.

Wachezaji wa Tottenham wanahofu juu ya mustakabali wa wa kocha wao Mauricio Pochettino, na wanaamini raia huyo wa Argentina anatafuta njia ya kuondoka klabuni hapo.

Manchester United pia wanaendelea kumfuatilia kiungo wa klabu ya Leicester na timu ya taifa ya England James Maddison, 22, ambapo wanaweza kumsajili kwa pauni milioni 80.(Mail)

Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kama sehemu ya kufufua kikosi cha Manchester United. (Manchester Evening News)

Baada ya kipigo kutoka Bayern, kocha wa Tottenham Pochettino alifanya mazungumzo ya dharura kwenye vyumba vya kubadili nguo, na aliendeleza mazungumzo hayo wakatii wa mazoezi jana Jumatano.

Toby Alderweireld, 30


Beki wa Tottenham Toby Alderweireld, 30, amekiri kuwa klabu hiyo imeporomoka kiwango zaidi sasa kuliko kipindi chochote katika miaka mitano iliyopita. Kikosi hicho kipo nyuma ya vinara wa ligi Liverpool kwa alama 10, wametolewa kwenye kombe la Corabao na klabu ya dara ja la pili Colchester na wakaadhibiwa vikali kwa goli 7-2 na Bayern Munich kwenye Champions League juzi Jumanne.

Kocha wa Arsenal Unai Emery amesema mshambuliaji wake raia wa Ivory Coast Nicolas Pepe anatakiwa kujifunza kustahamili presha ya kuwa mchezaji wa Arsenal. Pepe, 24, amesajiliwa na Arsenal kwa rekodi ya kitita kinono zaidi cha pauni milioni 72 mwezi Agosti akitokea klabu ya Lille.

Mshambuliaji wa England na Manchester City Raheem Sterling, 24, anaamini wakati wa klabu yake kushinda michuano ya Champions League umekaribia, japo amewaasa wachezaji wenzake kusalia na subira. (Mirror)

West Ham wamemkadiria thamani ya pauni milioni 80 kiungo wao Declan Rice, 20, kufuatia tetesi kuwa anatakiwa na klabu ya Manchester United.

Mshambuliaji fundi wa zamani wa Spurs na Manchester United Dimitar Berbatov anaamini mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy atafanya mazungumzo na Pochettino "wiki hii" ili "kupata majibu sahihi na njia muafaka ya kusonga mbele." (Star)

Chelsea wanampango wa kumsajili beki wa kati kinda kutoka klabu ya Monaco Benoit Badiashile, 18, mwezi Januari endapo watafanikiwa kuruhusiwa kufanya usajili. (Le 10 Sport)

Bayern Munich wanataka kumsajili mchezaji kinda na nyota wa Birmingham Jude Bellingham, 16, na kumfanya nyota wao wa baadae kutoka England.

Arsenal wanaweza kumsajili beki wa RB Leipzig Dayot Upamecano, 20, mwezi Januari kwa kitita cha pauni milioni 53 baada ya kushindwa kumnunua kwenye dirisha la usajili lililopita kwa kuishiwa bajeti. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Oktoba 3, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Oktoba 3, 2019 Reviewed by Zero Degree on 10/03/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.