Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Oktoba 23, 2019


Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Paris St-Germain na Juventus, Zlatan Ibrahimovic, 38, anataka kurejea katika ligi kuu ya Italia, Serie A.

Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Uswidi katika klabu ya LA Galaxy unakamilika mwisho wa mwaka huu. (CalcioMercato)

Mchezaji wa zamani wa Liverpool wa safu ya kati Dietmar Hamann anasema kuwa amepata fununu kwamba Reds "wanahamu sana" ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19. (Sky Germany)

Tottenham wana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania wa miaka 21 Carles Alena kutoka Barcelona mwezi Januari. (Mundo Deportivo)
Juventus na Atletico Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia beki wa West Brom Nathan Ferguson, 19.

Manchester United huenda ikaongeza juhudi ya kumsajili Mario Mandzukic, 30, baada ya mshambuliaji wa Juventus na Croatia kupunguza masharti ya marupu rupu yake. (Sun)

Brahim Diaz, 20

Klabu ya Real Madrid imemwambia kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City Brahim Diaz, 20, kwamba inataka kumuuza kama sehemu ya kuondokeana nae kabisa.

Mchezaji wa safu ya kati ya Real Madrid Isco, 27, amekubali kuwa mmoja wa wachezaji watakaoondoka klabu hiyo mwezi January mwakani. (Mail)

Barcelona imepinga madai kuwa imeilipa Atletico Madrid euro milioni 15 kumaliza mzozo kati yake na klabu hiyo kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28. (Sport)

Meneja wa chuo cha mafunzo ya soka ya Manchester United Nicky Butt anasema klabu hiyo inawachezaji wengi ambao wanaweza kufuata nyayo za mshambuliaji Marcus Rashford na kuleta mabadiliko katika kikosi cha kwanza. (Goal)

Crystal Palace itamenyana na Aston Villa katika juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos, 23, kutoka Rangers mwezi Januari.

Kocha wa zamani wa Tottenham Glenn Hoddle anadai kuna wachezaji "wanne au watano" katika kikosi cha Mauricio Pochettino ambao wanajua wataondoka katika klabu hiyo mwanzo wa msimu ujao. (Express)

Beki wa zamani wa Manchester United Jaap Stam ambaye anatarajiwa kujiunga na Feyenoord msimu huu wa joto anasema kuwa alikataa nafasi aliyopewa ya kuwa meneja wa Newcastle. (Voetbal International)

Newcastle imepinga madai hayo na kusisitiza kuwa haijawahi kuwa na mpango wa kumuajiri mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi. (Chronicle)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Oktoba 23, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Oktoba 23, 2019 Reviewed by Zero Degree on 10/23/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.