TFF yataja hatma ya Ndayiragije, Stars
Shirikisho la soka Tanzania TFF limezungumzia hatma ya Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije ikiwa katika harakati za kutafuta kocha wa kudumu wa timu hiyo.
Kupitia kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo, Oscar Mirambo, TFF imeshapokea jumla ya maombi takribani 200 ya makocha mbalimbali duniani na kueleza kuwa hatma ya kocha Ndayiragije itafahamika baada ya kukabidhi ripoti yake ya ufundi.
"Ndayiragije alipewa kazi ya kuivusha timu kwenye michuano ya CHAN ambayo inahusisha wachezaji wa ndani na ameliweza, kilichobaki sasa ni kupokea ripoti yake na kuifanyia kazi mambo mengine yatafuata baadaye kujua hatma yake kwani siyo suala la kukurupuka", amesema Oscar Mirambo.
Kuhusu maombi ya nafasi ya kuifundisha Stars, Mirambo amesema kuwa katika maombi yote waliyopokea mpaka sasa hakuna kocha yoyote mzawa aliyejitokeza kuomba nafasi.
“Tulitangaza nafasi kwa kocha mwenye uwezo wa kuinoa timu yetu na mwitikio umekuwa mkubwa kwa makocha wa kigeni, wengi wametuma barua za maombi ya kazi ikiwa ni zaidi ya barua 273 lakini Katika maombi hayo yote ya makocha hakuna jina la mzawa hata moja, hali ambayo inaonesha kuwa mwamko kwao umekuwa mdogo", ameongeza.
Etienne Ndayiragije ameiongoza Stars katika michezo mitano mpaka sasa tangu alipokabidhiwa timu, akishinda mechi moja, sare tatu na kufungwa mechi moja. Mafanikio makubwa aliyoipa Stars ni kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN, baada ya kuifunga Sudan.

Reviewed by Zero Degree
on
10/24/2019 08:18:00 AM
Rating: