Limao na nguvu za kiume
Madaktari wanasema limau ni moja ya tunda muhimu kwa mwili wa binadamu kutokana na virutubisho vyake.
Kuna aina tofauti ya limau katika maeneo tofauti duniani lakini iliyo na umaarufu zaidi ni yale malimau madogo yenye uchachu maalum, yanapatikana barani Afrika na Asia.
Jarida la Healthline lililoangazia kwa kina umuhimu wa limau kwa afya linasema lina madini ya Vitamin C, ambayo yanachangia asilimia 20 ya mahitaji ya binadamu mwilini.
Pia lina madini ya chuma, calcium, vitamin B, potassium na magnesium
Utafiti unaonesha kwamba kunywa juisi ya limau kunaimarisha kinga ya mwili, kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na figo na pia kunaimarisha afya ya ngozi.
Kuna wengine wanadai kunywa maji ya limau kunapunguza ashiki kwa wanaume na wanawake.
Kulingana na Hajia Jummai Hassan, mshauri wa chakula bora katika hospitali ya Wuce mjini Abuja, kando na manufaa mengine kwa afya limau linasaidia katika ukuzaji wa nguvu za kiume.
Anasema Limau lina matumizi tofauti lakini pia- linatumiwa kwa juisi na chakula pia.
"Watu wanafikiria ni hatari kwa wanandoa kutumia limau lakini hiyo ni dhana potovu. Kwa sababu utafiti unaonesha kuwa matumizi kiasi ya limau yanasaidia kuimarisha nguvu za kiume."
"Kiwango kidogo cha maji ya limau kikiwekwa katika maji ya kunywa ama kwenye chai hakiwezi kuathiri nguvu za kiume - bali kinatengeneza na kuziimarisha zaidi."
"Bila Shaka najua kunywa maji ya limau nusu kikombe - ni hatari kwa afya ya uzazi wa wanaume," anasema mtaalamu huyo wa masuala ya lishe bora.
Anasema kunywa maji mengi ya limau kunaweza kudhibiti ukuzaji wa nguvu za kiume kwa wale ambao hawataki tena kupata watoto.
Pia ameongezea kuwa utafiti uliofanywa nchini Australia umeonesha kuwa kunywa maji ya limau kwa wingi kunaweza kuathiri nguvu za kiume.
"Endapo utatumia maji ya limau kabla ya kufanya tendo la ndoa bila shaka nguvu za kiume zitaathirika."
Hufai kunywa maji mengi ya limau kwa wakati mmoja- Kitu chochote kikizidishwa huwa si kizuri lakini sio kibaya kwa wanandoa.
Juisi ya limau husaidia kutibu mafua na mwasho wa kooni
Maji ya limau pia yanapunguza kwa kiwango kikubwa uzani wa mwili.
Limau lina virutubisho muhimu kama vile madini ya Vitamin C, Potassium na Magnesium. Na linatumiwa kwa njia tofauti.
Madaktari wanashauri ikiwa unataka kutumia limau nyakati za asubuhi baada ya kuamka, ukate kipande kidogo na kukiloweka ndani ya maji ya moto ama chai kisha unywe baadae.
Kwa mujibu wa Dkt. Jummai, ni vyema kutumia limau kwenye maji badala ya kuweka kwenye kahawa, kwa sababu chembe chembe za limau ambazo hazijasagika huondoa kemikali mwilini kupitia mikojo.
Lakini limau likiongezwa kwenye maji litasalia mwilini hali ambayo itakuwa na manufaa kwa mwili.
Pia anapendekeza mtu kunywa maji ya limau asubuhi anapaomka mbali na kutumia anapokula samaki au kutengeza saladi.
Hajiya Jummai, mtaalamu wa lishe bora katika hospitali ya Wuse Hospital, anasema kutumia limau kunategemea afya ya mtu kwasababu kitu chochote ambacho ni kizuri kwa mtu mmoja huenda kikawa na madhara kwa mwengine.
Anasema kuna watu ambao miili yao inachagua vyakula filani.
Kuna wale ambao wakitumia juisi ya limau wanatapika na wengine hupata kiungulia, kwa mujibu wa data za jarida la afya la Healthline.
Jarida la Healthline lililoangazia kwa kina umuhimu wa limau kwa afya linasema lina madini ya Vitamin C, ambayo yanachangia asilimia 20 ya mahitaji ya binadamu mwilini.
Pia lina madini ya chuma, calcium, vitamin B, potassium na magnesium
Utafiti unaonesha kwamba kunywa juisi ya limau kunaimarisha kinga ya mwili, kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na figo na pia kunaimarisha afya ya ngozi.
Je uchachu wa limau unasaidia mbegu za kiume
Baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kunywa maji ya limau ni hatari kwa maisha yao ya ndoa, kwa sababu jamii za kitamaduni ziliamini kuwa maji hayo yanaathiri mbegu za kiume.Kuna wengine wanadai kunywa maji ya limau kunapunguza ashiki kwa wanaume na wanawake.
Kulingana na Hajia Jummai Hassan, mshauri wa chakula bora katika hospitali ya Wuce mjini Abuja, kando na manufaa mengine kwa afya limau linasaidia katika ukuzaji wa nguvu za kiume.
Anasema Limau lina matumizi tofauti lakini pia- linatumiwa kwa juisi na chakula pia.
"Watu wanafikiria ni hatari kwa wanandoa kutumia limau lakini hiyo ni dhana potovu. Kwa sababu utafiti unaonesha kuwa matumizi kiasi ya limau yanasaidia kuimarisha nguvu za kiume."
"Kiwango kidogo cha maji ya limau kikiwekwa katika maji ya kunywa ama kwenye chai hakiwezi kuathiri nguvu za kiume - bali kinatengeneza na kuziimarisha zaidi."
"Bila Shaka najua kunywa maji ya limau nusu kikombe - ni hatari kwa afya ya uzazi wa wanaume," anasema mtaalamu huyo wa masuala ya lishe bora.
Anasema kunywa maji mengi ya limau kunaweza kudhibiti ukuzaji wa nguvu za kiume kwa wale ambao hawataki tena kupata watoto.
Pia ameongezea kuwa utafiti uliofanywa nchini Australia umeonesha kuwa kunywa maji ya limau kwa wingi kunaweza kuathiri nguvu za kiume.
"Endapo utatumia maji ya limau kabla ya kufanya tendo la ndoa bila shaka nguvu za kiume zitaathirika."
Hufai kunywa maji mengi ya limau kwa wakati mmoja- Kitu chochote kikizidishwa huwa si kizuri lakini sio kibaya kwa wanandoa.
Baadhi ya manufaa ya limau kwa mwili
Juisi ya limau huua viini vya bakteria mdomoni na pia huondoa harufu mbaya mdomoniJuisi ya limau husaidia kutibu mafua na mwasho wa kooni
Maji ya limau pia yanapunguza kwa kiwango kikubwa uzani wa mwili.
Limau lina virutubisho muhimu kama vile madini ya Vitamin C, Potassium na Magnesium. Na linatumiwa kwa njia tofauti.
Madaktari wanashauri ikiwa unataka kutumia limau nyakati za asubuhi baada ya kuamka, ukate kipande kidogo na kukiloweka ndani ya maji ya moto ama chai kisha unywe baadae.
Kwa mujibu wa Dkt. Jummai, ni vyema kutumia limau kwenye maji badala ya kuweka kwenye kahawa, kwa sababu chembe chembe za limau ambazo hazijasagika huondoa kemikali mwilini kupitia mikojo.
Lakini limau likiongezwa kwenye maji litasalia mwilini hali ambayo itakuwa na manufaa kwa mwili.
Pia anapendekeza mtu kunywa maji ya limau asubuhi anapaomka mbali na kutumia anapokula samaki au kutengeza saladi.
Madhara ya limau kwa afya
Wataalamu wa afya wanasema kwamba limau lina manufaa mengi kwa mwili wa binadamu lakini pia halikosi kuwa na madhara kidogo hasa kwa wale walio na vidonda vya tumbo.Hajiya Jummai, mtaalamu wa lishe bora katika hospitali ya Wuse Hospital, anasema kutumia limau kunategemea afya ya mtu kwasababu kitu chochote ambacho ni kizuri kwa mtu mmoja huenda kikawa na madhara kwa mwengine.
Anasema kuna watu ambao miili yao inachagua vyakula filani.
Kuna wale ambao wakitumia juisi ya limau wanatapika na wengine hupata kiungulia, kwa mujibu wa data za jarida la afya la Healthline.
Chanzo: BBC
Limao na nguvu za kiume
Reviewed by Zero Degree
on
9/12/2020 02:18:00 AM
Rating: