17 wajeruhiwa Urusi kufuatia shambulizi la Ukraine
![]() |
| Jengo la makaazi katika mji wa Belgorod limeharibiwa katika shambulizi la kombora linalodaiwa kurushwa na Ukraine. |
Wizara ya ulinzi nchini Urusi, imesema kuwa kombora la Ukraine aina ya Tochka-U, lililenga eneo la makazi mjini humo baada ya kudunguliwa na mifumo ya ulinzi wa anga.
Murashko amenukuliwa na kituo cha habari cha serikali RIA Novosti akisema kwamba majeruhi hao 17 wamepelekwa kwenye vituo vya afya.
Wizara ya kukabiliana na hali za dharura imesema watu 12, wanaowajumuisha watoto wawili, wameokolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo.
Wizara hiyo pia imeonya kuwa idadi ya majeruhi inaweza kuongezeka kwa sababu sehemu ya paa la jengo hilo imeporomoka wakati maafisa wa uokoaji walipokuwa wakiwatafuta manusura.
Gavana wa Belgorod Viacheslav Gladkov amelaani mashambulizi hayo ya jeshi la Ukraine.
DW

Reviewed by Zero Degree
on
5/13/2024 11:22:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
5/13/2024 11:22:00 AM
Rating: