Zaidi ya watu 140 wafariki Brazil kwa mafuriko
Idadi ya vifo vinavyotokana na mvua iliyosababisha mafuriko katika Jimbo la Rio Grande do Sul huko nchini Brazil imeongezeka na kufikia watu 143, huku wengine 125 wakiwa hawajulikani walipo.
Mamlaka nchini Brazil imesema katika jimbo hilo la kusini mwa Brazil viwango vya maji kwenye mito inaripotiwa kupanda, huku Idara ya hali ya hewa ikisema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha "zinatia wasiwasi."
Mnamo siku ya Jumamosi, serikali ilitangaza kitita cha dola bilioni 2.34 kwa matumizi ya dharura ili kushughulikia janga hilo ambalo limesababisha zaidi ya watu 538,000 kuyahama makazi yao.
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesema serikali kuu itajenga upya miundombinu yote iliyoharibiwa na mvua katika jimbo hilo la Rio Grande do Sul.
Kwa upande wake, Rais Joe Biden wa Marekani amesema utawala wake unawasiliana na Brazil kwa lengo la kutoa msaada kwa waathiriwa wa mafuriko.

Reviewed by Zero Degree
on
5/13/2024 10:08:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
5/13/2024 10:08:00 AM
Rating: