Lori la mizigo lagonga hoteli
Mlinzi wa Hoteli moja mjini Njombe mkoani Njombe, Daniel Mlowe amenusurika kifo baada ya lori la mizigo kuacha njia na kisha kugonga hoteli iliyopo mjini hapa majira ya saa 11 alfajiri.
Akizungumza mara baada ya kunusulika kugongwa na lori hilo mlinzi aliyekuwa kibanda cha lindo lake hotelini hapo amesema huenda dereva wa gari hilo alikuwa na mwendo mkali kwasababu punde baada ya ajali alifanikiwa kumhoji na kuambiwa ametumia dakika 20 kutoka Mtwango hadi Njombe mjini penye zaidi ya Km 30.
Baadhi ya wakazi wa Njombe waliofika katika eneo la tukio muda mfupi baada ya kutoka akiwemo Kephas Agusto na John Mwalongo wamesema mazingira ya tukio hilo yanaonyesha dereva wa lori amekinzana na gari lingine huku wengine wakisema mwendo kasi au usingizi ndiyo chanzo.
Kwa upande wake, Abeli Luoga ambae ni dereva bodaboda anasema amekutana na tukio hilo majira ya saa moja asubuhi akipeleka mteja kituo cha basi.

Reviewed by Zero Degree
on
5/13/2024 06:45:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
5/13/2024 06:45:00 AM
Rating: