Loading...

Tanzia: Mtangazaji Swedy Mwinyi afariki Dunia


Mtangazaji mahiri wa vipindi wa michezo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Sued Mwinyi amefariki Dunia leo Mei 12, 2024 katika hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Dk. Ayub Rioba Chacha amethibitisha kutokea kwa msiba huo.

Mwinyi atakumbukwa kwa umahiri wake wakati wa matangazo ya mpira wakati ule akitangaza kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na baadaye TBC.

Pia amewahi kufanya kazi na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW). Mara ya mwisho ameonekana #mjengoni Aprili 2020 kwenye Jaramba la Wikiendi.
Tanzia: Mtangazaji Swedy Mwinyi afariki Dunia Tanzia: Mtangazaji Swedy Mwinyi afariki Dunia Reviewed by Zero Degree on 5/13/2024 07:21:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.