Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 15 Mei, 2024
Manchester United wako tayari kutoa pauni milioni 55, kumnunua beki wa Everton na England chini ya umri wa miaka 21 Jarrad Branthwaite. (Daily Mail)
Klabu ya Bayern Munich wana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United Bruno Fernandes msimu huu wa joto na wanaamini kuwa wanaweza kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 29 kwa sababu ya hali ya kufadhaika Old Trafford. (Independent)
Wachezaji kadhaa wakuu wa Bayern Munich akiwemo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane, 30, wanataka meneja Thomas Tuchel kubadili uamuzi wake wa kuondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga mwishoni mwa msimu huu. (Abendzeitung)
Mlinzi wa Uholanzi Jeremie Frimpong, 23, anaelekea kuondoka Beyer Leverkusen msimu huu wa joto huku Real Madrid, Manchester City, Arsenal na Manchester United zikiwa na nia ya kunufaika na kipengele cha pauni milioni 35 katika mkataba wake. (Bild)
Arsenal na Manchester City wamewasiliana na kiungo wa kati wa Newcastle United na Brazil Bruno Guimaraes, 26, kuhusu uwezekano wa uhamisho msimu wa joto. (Caughtoffside)
Mkufunzi wa klabu ya Brentford, Thomas Frank ni miongoni mwa makocha wanaotarajiwa kujiunga na Manchester United endapo wataamua kumfuta kazi meneja wao Erik ten Hag. (Telegraph)
Napoli wamempa mkufunzi wa zamani wa Chelsea na Tottenham Antonio Conte pauni milioni 5.6 kwa mwaka kuwa kocha wao ajaye lakini nia ya AC Milan ya kumnunua Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 54 imefifia. (Sport)
AC Milan wanamsaka beki mpya na beki wa Tottenham mwenye umri wa miaka 25 wa Brazil Emerson Royal yuko juu kwenye orodha yao ya wachezaji walioteuliwa. (Fabrizio Romano)
Klabu ya Manchester United wanamenyana na Newcastle United katika mbio za kumnunua beki wa Fulham Muingereza Tosin Adarabioyo, 26. (Talksport)
Liverpool wamepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Nice na Ufaransa Khephren Thuram, 23, kwa pauni milioni 13 msimu huu. (Mirror)
Mkufunzi wa Feyenoord Arne Slot anapanga kumfanya meneja wake msaidizi Sipke Hulshoff uteuzi wa kwanza wa wahudumu wake wa klabu ya Liverpool atakaporithi mikoba ya Jurgen Klopp. (ESPN)
Wolves wanatarajiwa kumpa meneja Gary O'Neil kandarasi mpya ya miaka mitatu. (i Sport)
Klabu ya Juventus wanataka kuachana na meneja Massimiliano Allegri mwishoni mwa msimu huu. (Rudy Galetti)
Aston Villa wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Gabri Veiga baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 wa Al-Ahli kuashiria kuwa ana hamu ya kurejea Ulaya msimu wa joto. (Givemesport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 15 Mei, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
5/15/2024 08:05:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
5/15/2024 08:05:00 AM
Rating:

