Wanafunzi 194 wabeba mimba ndani ya mwezi mmoja
NDANI ya muda wa mwezi mmoja jumla ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wapatao 194 wamebainika kupewa mimba na kukatishwa masomo yao katika wilaya ya Momba Mkoani Songwe.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Chiwanda wilayani humo.
Chongolo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Momba, Kenan Kihongosi, kuwatafuta na kuwachukulia hatua wale wote waliosababisha mimba hizo kwa watoto waliochini ya miaka 18 na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Hata hivyo ameagiza Mtendaji wa Kata ya Nkangamo na Mwenyekiti wa kijiji cha Chiwanda kutokubali kumaliza masuala hayo kienyeji, na watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwani wao ndio wanawatambua wananchi katika maeneo yao.

Reviewed by Zero Degree
on
5/15/2024 08:15:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
5/15/2024 08:15:00 AM
Rating: