Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 13 Mei, 2024


Liverpool wanavutiwa na winga wa Newcastle mwenye umri wa miaka 23 Anthony Gordon, ambaye alianza kucheza soka katika klabu ya Everton. (Star)

Mkataba wowote kwa Gordon unaweza kukatiza matumaini ya Arsenal ya kumsajili mshambuliaji wa Newcastle mwenye umri wa miaka 24 raia wa Uswidi Alexander Isak msimu huu wa majira ya joto. (Express)

Mshambuliaji wa Colombia Luis Diaz, 27, amepuuza tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kwenda Paris St-Germain, akisema "mambo mazuri yanakuja" Liverpool. (Mirror)

Sheffield United iko tayari kutoa ofa ya pauni milioni nane kwa mlinda mlango wa Sunderland Muingereza Anthony Patterson, 23.

Manchester City wanavutiwa na mlinda mlango wa chuo cha mafunzo ya soka ya Everton mwenye umri wa miaka 16 Douglas Lukjanciks na wanaweza kulipa hadi pauni milioni 10 kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza wa chini ya miaka 17. (Sun)

Newcastle wanapigiwa upatu kumsajili mlinzi Tosin Adarabioyo mwenye umri wa miaka 26 kwa uhamisho wa bure, wakati mkataba wake na klabu ya Fulham utakapokamilika msimu huu wa majira ya joto. (Mail)

Eintracht Frankfurt haitaanzisha mchakato wa pauni milioni 13 wa kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Uholanzi aliyeko kwa mkopo Donny van de Beek, 27.

Klabu ya Crystal Palace haitamruhusu meneja wa Austria Oliver Glasner, 49, kuondoka msimu wa joto, licha ya tetesi zinazomhusisha na nafasi ya ukocha mkuu katika klabu ya Bayern Munich. (Fabrizio Romano)



Luka Modric

Mustakabali wa Luka Modric utawekwa wazi "wiki ijayo", asema wakala wake, huku kandarasi ya kiungo huyo wa kati wa Croatia mwenye umri wa miaka 38 katika klabu ya Real Madrid ikikamilika msimu huu wa joto. (Goal)

Klabu za Everton, Brighton, Inter Milan na Wolfsburg wanapania kumnunua beki wa AZ Alkmaar raia wa nchi ya Japan Yukinari Sugawara, 23. (Florian Plettenberg)

Mkufunzi wa klabu ya Everton Sean Dyche ana matumaini ya kuchunguza mpango wa kubadilisha mkopo wa winga wa timu ya taifa ya Uingereza Jack Harrison kutoka Leeds kuwa uhamisho wa kudumu. (Liverpool Echo)

West Ham wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Sevilla raia wa Morocco, 26, Youssef En-Nesyri msimu wa joto. (Football Insider)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 13 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 13 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/13/2024 09:06:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.