Akili yetu sasa inaziwaza dakika 180 dhidi ya Vital'O - Kamwe
Baada ya droo iliyofanyika jijini Cairo nchini Misri juzi, ambapo Mabingwa wa Tanzania Bara, imepangwa kucheza dhidi ya Vital'0 ya Burundi, klabu ya Yanga imesema itakwenda kucheza na timu hiyo kwa tahadhari na wala hawatoidharau.
Klabu hiyo imesema ingawa baadhi ya wachambuzi wanaona kama timu hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni mchekea, lakini watakuwa makini kuelekea kwenye mchezo huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa timu hiyo, Ali Kamwe, amesema kwa sasa akili yao yote inaziwaza dakika 180 za mechi hiyo, ambazo kama wanapita ndizo zitawapa mwangaza kwa nini cha kufanya kwenye mchezo unaofuata.
"Droo tumeipokea vizuri, bahati nzuri imepangwa tukiwa tumeshaanza mazoezi yetu ya kwanza, hivyo tulikuwa tunaishuhudia kwa pamoja hapa Kigamboni pamoja na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi.
Kitu ambacho tumekubaliana na kusahau msimu mzuri ambao tumeupitia kwenye Ligi ya Mabingwa msimu uliopita ya kufika mpaka robo fainali, tumekubaliana kuanza upya, kuanza kuhesabu hatua zingine kwa sababu tuna ndoto za kufanya makubwa msimu unaokuja kwenye michuano hiyo, ikiwa ni pamoja na kupita hatua tuliyoiweka msimu uliopita," alisema Kamwe.
Alisema kutokana na hilo, wako makini sana na mchezo ambao watacheza dhidi ya Vital'0, ambao ndiyo utawapa mwanga wa nini watakwenda kukifanya msimu ujao
"Akili yetu sasa inaziwaza dakika 180 hizi dhidi ya Vital'O, tukishamaliza ndipo tutaanza kuangalia mchezo unaofuata utakuwaje," alisema.
Yanga inatarajiwa kuanza mechi yake ugenini, kati ya Agosti 16 hadi 18, huku mechi ya marudiano ikitarajiwa kuchezwa nyumbani kati ya Agosti 23 mpaka 25.
Yanga inaanzia raundi ya awali, ambapo kama itafanikiwa kupita, itakwenda moja kwa moja raundi ya kwanza na kucheza kukutana na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda na Commercial Sports ya Ethiopia.
Msimu uliopita, Yanga iliishia katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na kuondoshwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa mikwaju ya penalti 3-2, baada ya suluhu mechi zote mbili zilizochezwa nchini na baadaye Sauzi.
Wakati huo huo, klabu hiyo imemtangaza mchezaji Duke Abuya, raia wa Kenya, akitokea klabu ya Singida Black Stars.
Tayari mchezaji huyo ameshajiunga na wachezaji wengine wa Yanga walioanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Mabingwa na michuano mingine inayowakabili.
Abuya, anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na wakati mwingine winga, kabla ya kujiunga na Singida, aliwahi kuzichezea klabu za Mathare United, Polisi ya Kenya, Kariobangi Sharks zote za nchini Kenya na Nkana Red Devils ya Zambia.

Reviewed by Zero Degree
on
7/13/2024 07:45:00 AM
Rating: