Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 13 Julai, 2024
Kiungo wa kati wa Ufaransa Desire Doue, 19, anatazamiwa kuamua kati ya Bayern Munich na Paris Saint-Germain ikiwa ataondoka Rennes msimu huu wa joto. (Sky Germany)
Mshambuliaji wa zamani wa Italia, Manchester City na Liverpool Mario Balotelli, 33, anajadiliana kuhusu mpango wa kujiunga na Corinthians kama mchezaji huru, anasema mkurugenzi wa vijana katika klabu hiyo ya Brazil. (ESPN)
Barcelona wanakaribia kufikia hali ya kifedha ambayo itawawezesha kumnunua winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22, kulingana na mkufunzi wa La Liga Javier Tebas. (Sport)
Lyon wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa kundi la umri wa miaka 16 Alejandro Gomes Rodriguez kutoka Southampton.
Mlinda mlango wa Chelsea Mhispania Kepa Arrizabalaga, mwenye umri wa miaka 29, yuko kwenye mazungumzo na Al-Ittihad kuhusu kuhamia Saudi Arabia. (Athletic)
Newcastle wako tayari kufufua tena mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, mwenye umri wa miaka 27 baada ya mazungumzo ya awali na Everton kugonga mwamba.
Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua beki wa Italia na klabu ya Bologna Riccardo Calafiori mwenye umri wa miaka 22.
Mshambuliaji wa Tottenham na Jamhuri ya Ireland Troy Parrott, 22, anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa matibabu kabla ya kuhamia AZ Alkmaar. (Football Insider)
Klabu ya Napoli bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 31.
Kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 29, amekubali kuondoka Atletico Madrid na kujiunga na Sevilla. (Sky Sports)
Kocha wa zamani wa klabu ya Paris Saint-Germain Laurent Blanc anatarajiwa kuteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Al-Ittihad hadi Juni 2026. (Fabrizio Romano)
Tottenham pia wana nia ya kumleta Doue kaskazini mwa London. (Football.London)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 13 Julai, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
7/13/2024 07:55:00 AM
Rating: