Coastal Union imejipanga kimataifa – Kocha
Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union, David Omna amesema kuwa amejipanga vizuri kuhakikisha wanaanza vyema kwenye mchezo wao wa awali wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya FC Bravos ya Angola kutokana na mazoezi anayoendelea kuwapa wachezaji wake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Kocha huyo aliweka wazi kuwa amefanya usajili mzuri ambao anaamini utaleta mapinduzi makubwa katika mchezo huo.
"Malengo yangu ni kufanya vizuri kwenye mchezo wetu huo ili tusonge mbele na kwa usajili nilioufanya ninaamini tutapata matokeo mazuri,” alisema Omna.
Kocha huyo alisema msimu huu amesajili wachezaji wenye viwango vya juu na kudai wengi wao wana uzoefu na mashindano ya Kimataifa.
Aliongeza kuwa anaitumia michuano ya Kagame inayoendelea kama maandalizi ya mchezo huo, kwani wachezaji wake wanajifunza vitu vingi kutoka kwa timu zinazoshiriki.
"Michuano hii inanisaidia kuendelea kuangalia mapungufu na uwezo wa kila mchezaji kabla hatujasafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuweka kambi ya muda,” alisema Kocha huyo.
Alisema anawaomba Watanzania waendelee kuwaombea ili waweze kufanikisha malengo yao ili waipeperushe vizuri bendera ya Taifa.

Alisema kila kitu kinawezekana na kusema mpinzani wake ana wachezaji wazuri hivyo amewataka wachezaji wake kuwa na tahadhari kubwa.
Chanzo: Nipashe
Coastal Union imejipanga kimataifa – Kocha
Reviewed by Zero Degree
on
7/13/2024 12:06:00 PM
Rating: