Beleke atua Yanga kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja
Mshambuliaji wa TP Mazembe, Jean Othos Baleke ambaye alikuwa kwa mkopo kunako klabu ya Al Ittihad ya Libya amethibitisha kujiunga na Young Africans Sc kama mchezaji mpya klabuni hapo kwa msimu ujao wa 2024/25.
Kupitia Insta Story yake Baleke ameposti picha akiwa ndani ya uzi wa Yanga Sc ikiwa ni Taarifa ya moja ya chombo cha habari kilichothibitisha ujio wake Jangwani.
Nyota huyo anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na klabu hiyo baada ya kusitisha mkataba wake wa mkopo na miamba hiyo ya Libya na kujiunga na Wananchi.
Nyota huyo anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na klabu hiyo baada ya kusitisha mkataba wake wa mkopo na miamba hiyo ya Libya na kujiunga na Wananchi.
Mshambuliaji huyo wa ambaye amewahi kuitumikia Simba Sc, amejiunga na kambi ya mazoezi ya Wananchi licha ya kimya kingi juu ya utambulisho wake kama mchezaji mpya klabuni hapo.
Baleke ameripotiwa kujiunga na Mabingwa hao wa nchi kwa mkopo wa msimu mzima na anatarajiwa kutangazwa muda mfupi ujao kama mchezaji mpya klabuni hapo.
Beleke atua Yanga kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja
Reviewed by Zero Degree
on
7/12/2024 02:49:00 PM
Rating: