Mkuu wa Polisi nchini Kenya ajiuzulu
Inspekta Jenerali wa polisi nchini Kenya amejiuzulu kufuatia wiki kadhaa za maandamano yenye ghasia ambapo zaidi ya watu 40 waliuawa.
Mashirika ya haki za binadamu yameshutumu polisi kwa kuwapiga risasi makumi ya waandamanaji, baadhi yao kuwaua, na kuwateka nyara au kuwakamata mamia kiholela.
Maandamano yalizuka nchini Kenya katikati ya mwezi uliopita kupinga mapendekezo ya nyongeza ya ushuru. Waandamanaji walivamia bunge muda mfupi baada ya wabunge kupitisha mswada huo tata. Hatua ya Rais William Ruto kuiondoa ilifeli kuzima maandamano. Alivunja baraza la mawaziri siku ya Alhamisi.
Kuna mipango ya kuendelea na maandamano ya kuchochea mageuzi.
"Mhe. William Samoei Ruto, Ph.D, CGH, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, tarehe 12 Julai, 2024, amekubali kujiuzulu kwa Eng. Japheth N. Koome, MGH, kama mkuu waPolisi," sehemu ya taarifa hiyo imesema.
Chanzo: BBC
Mkuu wa Polisi nchini Kenya ajiuzulu
Reviewed by Zero Degree
on
7/13/2024 06:19:00 AM
Rating: