Loading...

TTCL kufikisha huduma ya mkongo wa mawasiliano DRC Congo


Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL limesema limeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi katika kutumia huduma za Interneti na kwaba mpaka sasa linaendelea na mchakato wa kufikisha huduma za mkongo wa taifa kwa nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) ikiwa ni muendelezo wa kupeleka huduma hiyo kwa nchi za jirani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 48 kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya TTCL (T-PESA), Lulu Mkudde amesema mpaka sasa huduma hiyo ya mkongo wa taifa imefikishwa katika nchi nne ikiwemo Burundi, Rwanda, Zambia na Malawi.

Amesema wanaposema wanafungua milango ya kidigitali wanamaanisha kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi katika kutumia huduma za Interneti katika kutekeleza huduma mbalimbali kwa watu wengine.

“Mpaka sasa shirika limefanya mambo mbalimbali ikiwemo huduma ya TTCL – Pesa ambapo katika Sabasaba hii tumekuja na huduma ya Akaunti Pepe inamuwezesha mteja kufungua akaunti yake bila hitaji ,mteja anauwezo wa kutumia akaunti yako masaa 24 kwa siku,”amesema.

Amesema mpaka sasa, Shirika limesambaza Mkongo wa Taifa katika mikoa yote nchini ambapo zaidi ya wilaya 98 zikiwa nazo zimefikishiwa Mkongo wa mawasiliano.


Mkudde amesema juhudi hizo zote zinalenga kuhakikisha juhudi za huduma za elimu, afya na Maendeleo ya kiuchumi ambayo yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini.

“Niwahakikishie TTCL ,itahakikisha huduma za mawasiliano inakuwa nzuri ili kuwapa fursa wananchi kupata huduma mbalimbali za kujipatia shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato kupitia fursa hii ya Interneti kwa gharama nafuu,”amesema

Akizungumzia Huduma ya T-cafe,Mkudde amesema huduma ya T -Café ni huduma ya WiFi ambayo ina waondolea adha wafanyabiashara, waandishi wa habari na wataalamu wa masuala ya ushauri katika kufanya kazi zao wakiwa nje ya ofisi.

Amesema ni huduma ambayo inasaidia mtu yoyote kufanya kazi nje ya ofisi kwa kupata uwezo wa kutumia huduma zao katika kutekeleza huduma zake .

“Shirika limeanzisha huduma hii ili kuwawezesha wateja wote kufanya shughuli zao kwa haraka na gharama nafuu,ambapo kwa kipindi hiki cha Sabasaba tumeshuhudia huduma hii inavyofanya kazi kwa speedi ya hali ya juu na wananchi kwa wakati wote walikuwa wakitumia katika maonesho hayo,”amesema.

Aidha amesema kupitia maonesho haya,TTCL imepata fursa ya kutoa elimu na kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu huduma hiyo wanayoitoa ambayo inamfikia mwananchi moja kwa moja .

“Tumepokea maombi mengi wateja wanahitaji huduma hii kwani yameleta mapinduzi ya kuisha haraka kwa vifurushi vya kawaida ambavyo shirika limeleta huduma hii kumuwezesha mwananchi kutumia Internet bila kikomo,”amesema.

Amesisitiza kuwa huduma yao hiyo haina ukomo na inatoa majibu kwa mtumiaji na kupunguza mlaji wa mwisho ukali wa gharama za ununuzi wa vifurushi.

“Nitumie nafasi hii kuwasihi wananchi ambao hawajaomba huduma hii wafike ofisini au wajngie katika tovuti yetu inayopatikana kisha tutachukua taarifa zao na kisha watahakikisha wanawafikishia huduma hii bure bila malipo,” amesema.
TTCL kufikisha huduma ya mkongo wa mawasiliano DRC Congo TTCL kufikisha huduma ya mkongo wa mawasiliano DRC Congo Reviewed by Zero Degree on 7/13/2024 07:19:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.