Brazil bado wanamtolea macho Carlo Ancelotti
Mnamo mwezi Desemba 2023, meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti alitia saini ya nyongeza ya kandarasi nyingine, na hivyo kuimarisha nafasi yake na klabu hiyo hadi mwaka 2026. Hata hivyo, hii haijawazuia Brazil kuendelea kumfuatilia Muitaliano huyo, anaripoti Alejandro Alcazar kupitia SPORT.
Kufuati timu ya taifa ya Brazil kutofany vizuri hivi majuzi katika michuano ya Copa America, ambapo walishindwa na Uruguay katika robo fainali kumezua hasira kubwa, huku shutuma nyingi zikilengwa kwa kocha Dorival Junior.
Licha ya hayo yote, Ednaldo Rodrigues, rais wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF), amethibitisha kuwa Dorival atasalia katika nafasi yake hadi mwaka 2026.
Rodrigues alisisitiza kwamba hakuna haraka ya kutafuta mbadala wake, akitaja mechi zijazo za kufuzu kwa Kombe la Dunia kama sababu ya kuendelea. "Baada ya miezi miwili, kuna mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia, na mpango ni kuendelea naye," alisema.
Brazil wanataka Ancelotti ayumbe Real Madrid Inafurahisha, baadhi ya waangalizi wanaamini mkakati huu ni njia ya kusigezaa wakati mbele, wakitumaini kwamba labda Ancelotti anaweza kukabiliwa na changamoto katika klabu ya Real Madrid, ambayo inaweza kumsababishia kuondoka mapema na uwezekano wa kuhamia Brazil.
Ikiwa Ancelotti atakumbana na changamoto huko Madrid, huenda akaishia kuihama klabu hiyo na kuinoa timu ya taifa ya Brazil, hivyo kuamsha mpango huo ambao awali ulitatizwa na kuongezewa mkataba.
Kinyume chake, ikiwa Ancelotti atafanya vyema akiwa na Madrid, huenda Brazil itashikamana na Dorival. Nyongeza ya mkataba wa Ancelotti na Real Madrid inatarajiwa kudumu hadi mwaka 2026, kulingana na mwisho wa kandarasi ya sasa ya Dorival, ambayo inaweza kumfanya Ancelotti kuchukua usukani wa timu ya taifa ya Brazil kwa wakati wa Kombe la Dunia la FIFA.
Brazil wanajua wanachokifanya
Kwa wakati huu, Rodrigues anasalia na tumaini la kuona matarajio ya Brazil chini ya Doriva ambaoyo ni pamoja na lengo lao la kufuzu michuano ya Kombe la Dunia yakitimia.
Hali hii inatengeneza picha ya kuvutia mno. Kwa upande mmoja, mustakabali wa Ancelotti katika klabu ya Real Madrid unaonekana kuwa salama kwa sasa, lakini kivutio cha kuinoa timu ya taifa ya kifahari kama Brazil bado kinabaki. Kwa upande mwingine, imani ya Brazil kwa Dorival inaashiria kujitolea kwa utulivu na mipango ya muda mrefu, licha ya vikwazo vya hivi karibuni.
Michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia inapokaribia, macho yote yatakuwa kwa Ancelotti na Dorival. Kiwango cha Ancelotti katika klabu ya Real Madrid kitachunguzwa sio tu na klabu yake bali pia na maafisa wa soka wa Brazil na mashabiki. Wakati huo huo, Dorival atakuwa na kazi ya haraka ya kuiongoza Brazil kupitia mchujo, na utendakazi wake unaweza kuamua kama mkakati wa muda mrefu wa CBF utaendelea kumshikilia au kuhama.
Brazil bado wanamtolea macho Carlo Ancelotti
Reviewed by Zero Degree
on
7/21/2024 07:12:00 AM
Rating: