Loading...

Vijana waitaka Serikali kuongeza Ajira

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema Vijana wengi wa Tanzania wamependekeza Serikali kushughulikia zaidi uchumi na ustawi wa jamii, kwa kuongeza nafasi za ajira na uwekezaji kwenye huduma bora za kijamii.

Prof.Kitila ametoa kauli hiyo leo July 20, 2024 Jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Kikanda la maandalizi ya dira ya maendeleo ya mwaka 2050 na kusisitiza kuwa zaidi ya asilimia 81 ya waliotoa maoni yao kufikia sasa kwenye kuandaa dira hiyo ya maendeleo ni Vijana kutoka maeneo mbalimbali.

Waziri Kitila Mkumbo ametaja vipaumbele vingine vilivyotajwa na Wananchi waliotoa maoni yao kuwa vimekuwa ni uimarishaji wa sekta ya Kilimo, Viwanda, Utalii na miundombinu mingine ya kijamii, akisisitiza umuhimu wa Wananchi kuendelea kutoa maoni yao kwa njia mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maelekeo ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.

Waziri Kitila amemwambia Mgeni rasmi Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Doto Biteko kuwa asilimia 69 ya Wananchi wanasema Nchi ipo kwenye muelekeo sahihi huku zaidi ya asilimia 76 wakisema miaka 25 ijayo nchi itakuwa kwenye eneo zuri zaidi kutokana na kasi ya utekelezaji wa mipango mbalimbali.

Akiongelea utekelezaji wa dira iliyopita, Waziri Kitila ametoa mfano wa ujenzi wa miundombinu akisema kuwa mwaka 1999 Tanzania ilikuwa na mtandao wa barabara wa Kilomita 85,000 pekee na kufikia 2022 Serikali imetekeleza mpango wake na kuwa na mtandao wa barabara wa Kilomita 181,190 sawa na ongezeko la asilimia 181.
Vijana waitaka Serikali kuongeza Ajira Vijana waitaka Serikali kuongeza Ajira Reviewed by Zero Degree on 7/21/2024 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.