Necta yafanya mabadiliko mfumo wa mitihani darasa la saba
Licha ya Serikali kubadili mfumo wa utahini kwa masomo sita ya elimu ya msingi likiwemo hesabu, wadau wa elimu wamesema juhudi hizo zifanywe pia katika kuwaandaa walimu wawe na umahiri wa kufundisha masomo hayo.
Ingawa kumekuwa na mapokezi chanya ya mabadiliko hayo, baadhi ya wadau wameonyesha upinzani hasa katika mtihani wa hesabu, wakisema unalazimu kumpima mwanafunzi kwa mtindo mmoja, ilhali uwezo na uelewa wao ni tofauti.
Wamekwenda mbali zaidi na kueleza, kulipaswa kuwepo na mitindo mbalimbali ya maswali ili isimchoshe mwanafunzi kujibu kwa namna moja.
Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), ule utaratibu wa mtihani wa hesabu kuwa na majibu ya kuchagua hautakuwepo tena, badala yake mwanafunzi atapaswa kukokotoa hesabu.
Mbali na hesabu, masomo mengine ni Kiswahili, Maarifa, Kiingereza, Sayansi na Uraia.
Taarifa kuhusu mabadiliko hayo imetangazwa jana Ijumaa, Julai 19, 2024 na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Said Mohamed, aliyesema mtihani wa somo la Hisabati utampasa mwanafunzi kukokotoa na kuandika majibu sahihi katika maswali yote.
“Lengo la maboresho haya ni kuimarisha utahini wa umahiri kuhakikisha wahitimu wanapata umahiri, weledi, uwezo wa kufikiri na maarifa na ujuzi utakaowawezesha kuwa na msingi imara wa elimu,” ameeleza.
Kwa mujibu wa Dk Mohamed, sambamba na hisabati, katika mitihani mingine wanafunzi watapimwa kwa aina mbalimbali za utahini, ikiwemo maswali ya kuchagua, kuoanisha, majibu mafupi, kupanga maneno na sentensi na kutafsiri picha.
Hata hivyo, alieleza maboresho hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maoni ya wadau juu ya mbinu za kuboresha mbinu za utahini.

Katika maboresho hayo, maswali yatapungua kutoka 45 hadi sita au nane na vipengele kati ya 33 hadi 38
Walichokisema wadau
Akizungumza na Mwananchi, Mwanazuoni wa Nadharia na Vitendo katika Mitalaa wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (Duce), Dk Josta Nzilano amesema mabadiliko hayo yanaunda mtindo mmoja pekee wa kumpima mwanafunzi katika mtihani.
Lakini kiuhalisia kwa mujibu wa Dk Ndilano, kulipaswa kuwa na mitindo zaidi ya mmoja wa kuwapima wanafunzi katika mtihani hasa wa hesabu.
Katika mtihani mmoja, alieleza kunapaswa kuwa na mitindo mbalimbali ya kumpima mwanafunzi, akimaanisha aina mbalimbali ya maswali yanayopaswa kujibuwa kwa njia tofauti.
“Kuwa na maswali yenye mtindo tofauti ina maana sana kulingana na akili ya mtoto na uwezo wake. Kuna mwingine anapimwa zaidi kwenye maswali ya kukokotoa na wapo wale wenye uwezo wa kujua majibu lakini hawezi kujieleza, wote wanajua isipokuwa wanatofautiana uelewa,” amesema.
Kwa mujibu wa Dk Nzilano, kunatakiwa kuwa na maswali mengi ya mtindo tofauti na kipimo kiwe ni kwa kiasi gani mtahiniwa amejibu maswali ya aina gani zaidi.
“Mabadiliko haya pengine ni hofu ambayo wataalamu wameona kwamba pengine watoto watakuwa wakipata majibu kwa kuhisia, lakini si sawa,” amesema.

Kinachotakiwa, amesema wanaoandaa mtihani walipaswa kupewa mafunzo ya kutunga maswali thabiti yanayopima mwanafunzi uwezo wa kutenda.
“Wapewe mafunzo, sio suala la kuondoa maswali, hapo tunajenga tatizo lingine kwa sababu watoto hawana uwezo sawa, kuna mwingine ana uwezo sana wa kujieleza mwingine hana uwezo wa kujieleza,” amesema.
Kwa upande mwingine wanazuoni hao wameyaona mabadiliko hayo kama majibu ya kilio cha muda mrefu cha wadau wa elimu juu ya mfumo wa utahini, kama inavyoelezwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St. John, Shadidu Ndosa.
“Maswali yanayotaka majibu ya kuchagua ni wazi yanapima kumbukumbu pekee, mtihani unapaswa kupima kumbukumbu, uwezo wa kufiki na kuchambua mambo. Kinachoenda kufanyika sasa kitakidhi sifa hizo za mtihani.
“Mfumo huu utatuwezesha kujua kwa usahihi viwango vya wanafunzi wetu wanaohitimu darasa la saba, uwezo wa mwanafunzi unaonekana pale anaposhughulisha akili yake kutafuta majibu sio kubahatisha kama ambavyo imeonekana kwa miaka ya karibuni,” alisema Ndosa.
Aina hiyo ya upimaji kwa mujibu wa Ndosa, itasaidia kupunguza uwezekano wa wizi au kuvujishwa kwa mitihani matukio ambayo yamekuwa yakibainika katika kila mitihani ya taifa inapofanyika.
Kwa mtazamo wa mhadhiri huyo, mfumo huo utazifanya shule kuja na mbinu thabiti za kuandaa wanafunzi kuelewa wanachofundishwa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo nguvu kubwa iliwekwa kwenye kujibu mitihani.
‘Hesabu za kukokotoa nzuri’

Kwa upande wake mdau wa elimu, Ochola Wayoga amesema mabadiliko hayo ya mfumo wa utahini yalitakiwa kufanyika kwa muda mrefu kwa kuwa hakuna namna mwanafunzi angepimwa uwezo wake wa kufanya hesabu kwa maswali ya kuchagua.
“Hesabu ni lazima mtoto afundishwe kukokotoa ili kupata majibu, sasa huo utaratibu wa kuchagua uliwekwa ili kupunguza kelele za watu yalipokuwa yanatoka matokeo kwa kuwa ilionekana kuna wanafunzi wengi walifeli somo hili.
Kabla ya maswali ya kuchagua mtihani wa hesabu ulikuwa wa kukokotoa, ufaulu ulikuwa hauzidi asilimia 20 sasa ikatafutwa njia ya kukabiliana na hilo ndiyo yakaja maswali ya kuchagua ambayo kwa hakika haikuwa njia sahihi. Ni heri sasa tunarudi kwenye mstari.”
Hata hivyo Wayoga alisema mabadiliko ya mfumo wa mitihani pekee hayawezi kuwa na tija kama hautafanyika uwekezaji mkubwa kwenye kutengeneza walimu wenye umahiri katika kufundisha hesabu.
“Ili mwanafunzi aelewe ni lazima afundishwe na mwalimu mwenye umahiri katika somo husika, sasa je hao walimu tulionao wanaandaliwa vyema? Jibu ni hapana ndiyo maana kilio cha kufeli hesabu kimeendelea kuwa kikubwa”alisema Wayoga.
Hoja hiyo ya maandalizi ya walimu imeelezwa na Ndosa ambaye alisisitiza kuwa mfumo wa kuwaandaa walimu unapaswa kujengewa msingi mzuri tangu chini ili kuwapata watu wanaoweza kuhamisha maarifa kwa wengine.
“Suala la hesabu ni tatizo la muda mrefu, suluhu yake inapaswa kuanzia chini kabisa huko kwenye kuwaandaa wanaobeba jukumu la kufundisha somo hili” alisema Ndosa.

Majibu ya Serikali
Akijibu hayo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo amesema wakati wote walimu wameandaliwa kufundisha kwa mbinu za ukokotoaji hasa katika somo la hisabati.
Mbinu hizo hizo, alieleza ndizo zinazotumika na walimu kufundisha darasani na kwamba haikuanza sasa ni utaratibu wa muda mrefu.
“Hili la maandalizi ya walimu kufundisha kwa njia ya ukokotoaji sio jipya, ni muda mrefu sana wamekuwa wakiandaliwa kwa utaratibu huo na wanafundisha hivyo darasani. Hata wewe (mwandishi) bila shaka ulifundishwa hesabu kwa kukokotoa,” alisema.
Kwa mujibu wa Profesa Nombo, kuna wakati mfumo wa utahini ulibadilika na hivyo kukinzana na utaratibu wa ufundishaji, akiurejea utaratibu wa kuweka majibu ya kuchagua katika somo la hesabu.
Lakini, kinachofanywa sasa kwa mujibu wa Profesa Nombo, kinaendana na mfumo wa ufundishaji, kadhalika matakwa ya sera na mitalaa ya elimu.
Sambamba na hilo, mtendaji mkuu huyo wa wizara hiyo, alisema msingi wa uamuzi huo ni kuwajenga wahitimu wawe na fikra tunduizi.
“Kusema ukweli fikra tunduizi ni zao la hesabu hasa mtoto akijua kukokotoa anakuwa na fikra tunduizi na ndiyo sababu ya mabadiliko haya. Tunataka watoto wawe na uwezo wa kifikra,” alieleza Profesa Nombo.
Chanzo: Mwananchi

Reviewed by Zero Degree
on
7/21/2024 06:12:00 AM
Rating: