Rais Ruto atangaza baraza la mawaziri 11
Rais William Ruto ametangaza mawaziri kumi na moja kati ya 22 katika baraza lake la mawaziri.
Katika hotuba yake kwa taifa , rais Ruto amesema kwamba idadi ya mawaziri waliosalia itatangazwa wiki ijayo baada ya mashauriano.
Haya yanajiri baada ya shinikizo kuongezeka kwa Rais kuchagua watu wenye uwezo ambao watamsaidia kutekeleza ajenda yake.
Rais amesema kwamba uteuzi huo ambao ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali - unafuatia mashauriano katika sekta ya kisiasa katika jaribio la kurudisha amani na utulivu nchini.
Orodha hiyo pia ilikuwa na Mawaziri sita waliofukuzwa kazi, ambao sasa wanarejea katika wizara tofauti, huku Prof. Kithure Kindiki, Alice Wahome na Adan Duale wakiendelea kushikilia nafasi zao za zamani.
Mawaziri walioteuliwa ni:
- Kithure Kindiki - Waziri wa masuala ya Ndani
- Dkt. Debra Mulongo Barasa - Waziri wa Afya
- Alice Wahome - Waziri wa Ardhi
- Aden Duale - Waziri wa Ulinzi
- Davis Chirchir - Waziri wa Uchukuzi
- Rebecca Miano - Mwanasheria Mkuu
- Soipan Tuya - Waziri wa Mazingira
- Julius Migosi - Waziri wa Elimu
- Eric Muriithi - Waziri wa Maji
- Dr Margaret Ndungu- Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia
- Andrew Karanja - Waziri wa Kilimo
"Ninaendelea kufanya mashauriano katika sekta mbalimbali kuhusu usawa wa Baraza la Mawaziri ambalo nitaliteua hivi karibuni. Mashauriano yapo katika hatua ya juu na michakato ya ndani katika sekta mbalimbali inaendelea ili kuwezesha uteuzi wangu wa uwiano wa Baraza hili la Mawaziri,” alisema Rais.
Rais Ruto atangaza baraza la mawaziri 11
Reviewed by Zero Degree
on
7/19/2024 03:14:00 PM
Rating: