Gamondi: Timu nzuri ni yenye uwezo uwanjani, sio majina ya wachezaji
Mkufunzi wa Yanga SC Miguel Gamondi amesema anategemea kuwa na msimu mgumu zaidi kwenye msimu mpya wa mashindano 2024-2025 kutokana na maandalizi ya klabu zingine kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajia kuanza Agosti 16-2024.
“Tuna kikosi kikubwa chenye wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini sitaki kusikia kuhusu Galacticos popote duniani timu nzuri ni yenye uwezo uwanjani na sio kwenye majina ya wachezaji na watu wetu wengi wanadhani tutakuwa na msimu mwepesi lakini nategemea kuwa na msimu ujao kuwa mgumu zaidi kutokana na klabu zingine kufanya maandalizi mazuri pamoja na kufanya usajili wa wachezaji wazuri na hili ni maendeleo kwa soka Tanzania” amesema Miguel Gamondi.
Kwa upande mwingine Kiungo Mshambuliaji wa Yanga SC Stephane Aziz Ki amesema anafurahishwa na ujio wa nyota Clatous Chama kutoka Simba SC na Prince Dube kutoka Azam FC kwani itasaidia kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao.
“Najisikia furaha kucheza na Chama na Dube ambao wamekuwa na misimu bora hapo nyuma ni furaha kuwa nao ndani ya timu moja ni jambo jema kwa kuwa tutakuwa na muendelezo mzuri wa kucheza vizuri kwa kuwa tunakuwa na wachezaji wengi wazuri ndani ya timu” alisema Aziz Ki.
Gamondi: Timu nzuri ni yenye uwezo uwanjani, sio majina ya wachezaji
Reviewed by Zero Degree
on
7/19/2024 01:48:00 PM
Rating: