Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 20 Julai, 2024

Victor Osimhen, 25

Chelsea haijakata tamaa katika harakati za kumsaka mshambulizi wa Napoli Victor Osimhen, 25, licha ya Paris St-Germain kuwa mstari wa mbele kumnasa mshambuliaji huyo wa Nigeria. (CaughtOffside)

Kiungo wa kati wa Uhispania Sergi Roberto, mwenye umri wa miaka 32, anajaribu kuhamia Ligi ya Preimia baada ya mkataba wake na Barcelona kumalizika. (Mundo Deportivo)

Crystal Palace wako tayari kutoa pauni milioni 30 kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Emile Smith Rowe, mwenye umri wa miaka 23. (Talksport)

Crystal Palace wamefanya mazungumzo ya awali na Marseille kuhusu uwezekano wa kumsajili winga wa Senegal Ismaila Sarr, 26.

Chelsea imemrejesha kiungo wa kati Lesley Ugochukwu mwenye umri wa miaka 20 kutoka katika kikosi cha Ufaransa cha Olimpiki huku kukiwa na mipango ya kumtoa kwa mkopo msimu huu. (Athletic)

Matias Soule, 21

Leicester wametuma dau lililoboreshwa la pauni milioni 21 kumnunua winga wa Juventus Matias Soule, 21, na wanatumai kukamilisha makataba wa Muargentina huyo wiki ijayo.

Chelsea wanataka kumsajili mlinda mlango mpya kuchuana na Mhispania mwenye umri wa miaka 26 Robert Sanchez . (Telegraph)

Chelsea wamepata ujumbe Newcastle kuhusu kupatikana kwa winga wa Uingereza Noni Madueke, 22.

Klabu ya Liverpool wako tayari kumuuza mlinda mlango wa Ireland, Caoimhin Kelleher, 25 iwapo watapata ofa inayofaa. (Football Insider)

Newcastle wanatumai kuwapiku West Ham na Juventus katika kumsajili mlinzi wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24, baada ya kufanya mazungumzo na Nice.

Anthony

Manchester United wako tayari kumruhusu fowadi wa Brazil Antony, 24, kuondoka kwa mkopo msimu huu wa kiangazi lakini iwapo tu klabu iko tayari kulipa mshahara wake wa £70,000 kwa wiki. (ESPN)

Mshambulizi wa Brazil Richarlison, 27, yuko tayari kujiunga na Saudi Pro League lakini Tottenham itadai £60m. (HITC)

Liverpool na Newcastle ni miongoni mwa vilabu vinavyohitaji kumnunua beki Mholanzi Dean Huijsen, 19, lakini thamani ya Juventus ya £25.3m inaweza kuwa kikwazo. (Tuttosport)

Kiungo wa kati wa Sheffield United Gustavo Hamer, 27, ana kipengele kinachomruhusu kuondoka katika kandarasi yake na Mbrazil huyo yuko anasakwa na vilabu kadhaa vya Premier League na Serie A. (Teamtalk).

Brighton wanatazamia kuendeleza mazungumzo kuhusu mkataba wa winga wa Kijerumani Brajan Gruda mwenye umri wa miaka 20 kutoka Mainz. (Fabrizio Romano)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 20 Julai, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 20 Julai, 2024 Reviewed by Zero Degree on 7/20/2024 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.