Makonda adaiwa kukiuka haki za binadamu
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetoa matokeo ya uchunguzi wa malalamiko yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kuhusu viongozi kadhaa, akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.
Uchunguzi huo umehusisha malalamiko 14 ikiwamo dhidi ya Makonda, aliyelalamikiwa kutoa amri ya kukamatwa na kuwekwa mahabusu mkazi wa mkoani humo kinyume cha utaratibu na sheria Juni, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, akitoa taarifa ya uchunguzi wa malalamiko hayo kwa waandishi wa habari jana Jualai 19, alisema jumla ya malalamiko 14 yaliyowasilishwa yamefanyiwa uchunguzi.

Alisema katika uchunguzi dhidi ya Makonda, THBUB imebaini kuwa amri iliyotolewa haikuwa halali na haikuzingatia aina ya makosa na utaratibu ulioainishwa kisheria wa utekelezaji wa mamlaka hayo.
“Na kwamba mwananchi huyo hakuwa mhusika wa madai ya msingi ambayo mkuu wa mkoa huyo aliyatumia kushughulikia suala lililokuwa mbele yake.
“THBUB imebainika kuwa pia, Makonda alivuka mipaka ya majukumu yake kwa kushughulikia na kutoa uamuzi katika suala ambalo lilipaswa kufuata mkondo wa kisheria wa kimahakama kwa kuwa madai hayo yangeshughulikiwa huko,” alisema.
Jaji Mstaafu Mwaimu alisema hata kama kulikuwa na viashiria vya makosa ya jinai, njia sahihi ingekuwa kulielekeza Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
“Na kwamba mwananchi huyo hakuwa mhusika wa madai ya msingi ambayo mkuu wa mkoa huyo aliyatumia kushughulikia suala lililokuwa mbele yake.
“THBUB imebainika kuwa pia, Makonda alivuka mipaka ya majukumu yake kwa kushughulikia na kutoa uamuzi katika suala ambalo lilipaswa kufuata mkondo wa kisheria wa kimahakama kwa kuwa madai hayo yangeshughulikiwa huko,” alisema.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu. |
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu.“THBUB pia ilibaini kutozingatiwa kwa haki za mtuhumiwa kwa kuwekwa mahabusu kwa saa 96 (yaani siku nne) bila kufunguliwa mashtaka," alisema Jaji Mwaimu.
Kadhalika alisema pamoja na mkuu huyo wa mkoa kuitwa mbele ya THBUB ili kuwasilisha utetezi wake alikaidi kufanya hivyo.
Chanzov Nipashe
Makonda adaiwa kukiuka haki za binadamu
Reviewed by Zero Degree
on
7/20/2024 10:09:00 AM
Rating: