Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 15 Julai, 2024
Manchester City watafanya mazungumzo na mchezaji wao wa kimataifa wa Argentina Julian Alvarez, 24, baada ya Copa America. Paris St-Germain wanavutiwa na mshambuliaji huyo, ambaye anataka muda zaidi wa kucheza, lakini City wanataka kusalia naye.
Manchester United imemsajili mshambuliaji wa Bologna na Uholanzi Joshua Zirkzee kwa mkataba wa thamani ya £36.54m.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ametia saini mkataba wa miaka mitano Old Trafford, na chaguola kuuongeza kwa miezi 12 zaidi.
Marc Guehi anasakwa na Liverpool, ambao wameanza mazungumzo ya kumsajili beki huyo wa kati wa Crystal Palace na England mwenye umri wa miaka 24. (Fabrizio Romano)
Liverpool wamemweka mlinzi wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Goncalo Inacio, 22, kuwa mlengwa wao mkuu katika kipindi cha uhamisho. (CaughtOffside)
Juventus wanamtaka kiungo wa kati wa Atalanta Mholanzi Teun Koopmeiners, mwenye umri wa miaka 26, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Liverpool. (Rudy Galetti)
Wolves wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua mlinzi wa Sheffield United mwenye thamani ya pauni milioni 20 Anel Ahmedhodzic, 25, kuchukua nafasi ya Muingereza Max Kilman, 27, aliyejiunga na West Ham.
Lakini kiungo wa kati wa Uingereza Adam Wharton, 20, atakataaofa kutoka Manchester City , Bayern Munich na Real Madrid ili kusalia Crystal Palace (Sun)
Arsenal wanapigiwa upatu kushinda Aston Villa katika harakati za kumnunua kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Mikel Merino, 28, msimu huu. (Mundo Deportivo)
Arsenal wamefikia makubaliano ya kumsajili mlinda lango wa kimataifa wa Uingereza Tommy Setford, 18, kutoka Ajax. (Athletic)
Klabu ya Manchester United iko tayari kumsajili mshambuliaji wa Norway Elisabeth Terland, 23 kutoka Brighton. (Guardian)
Jakub Kiwior ataruhusiwa kuondoka Arsenal msimu huu wa joto na beki huyo wa Poland mwenye umri wa miaka 24 anavutiwa na vilabu kadhaa vya Serie A. (Football Insider)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 15 Julai, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
7/15/2024 08:10:00 AM
Rating: