Wapeni nafasi watoto wa kike waweze kusoma na kutimiza malengo yao - Rais Samia
Watoto wamejifungua watoto: Sasa wanabeba majukumu yanayokiuka sheria - mtoto kulea mtoto mwenziwe; Sheria ya Ulinzi wa Mtoto, 2009 imekiukwa.
Ni jambo lililomshtua Rais Samia Suluhu Hassan jana alipobaini kuwapo idadi kubwa ya watoto wanaojifungua wakiwa chini ya umri wa miaka 19 mkoani Katavi.
Baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Katavi na kutembelea wodi ya wazazi ya hospitali hiyo, Mkuu wa Nchi alibaini kuwapo wazazi waliojifungua ambao wana umri wa kati ya miaka 15 na 19.
"Wakati ninatembea kwenye hospitali hii, nilipita kwenye hodi ya kinamama wanaojifungua na hasa wale watoto ambao hawajatimia (njiti).
"Nimekuta mama mmoja tu ndiye aliyepevuka, ana miaka 22, lakini wengine wote wapo kati ya miaka 15 na 19 na hawa ndio wanajifungua watoto ambao hawajatimia.
"Ninaomba sana wananchi wa mkoa huu wa Katavi, wapeni nafasi watoto wa kike waweze kusoma na kutimiza malengo yao na hata wafikie umri unaostahili angalau ajifungue akiwa amefikia umri wa miaka 19 na kuendelea, siyo hali hii niliyoikuta hapa, hii siyo sawa.
"Ujumbe huo ni kwenu wananchi mliopo hapa na wale ambao wananisikiliza kupitia vyombo vya habari, tujitahidi kuwapa nafasi watoto wa kike wapate elimu, wapevuke kabla ya kuolewa au kupewa ujauzito, hilo ninaomba sana sana," Rais aliagiza.
Rais Samia pia alipongeza alichokitaja "kazi nzuri iliyofanywa kwa kujenga hospitali inayokidhi vigezo vya kuwa ya rufani".
Kwa mujibu wa Rais Samia, hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa sawa na hospitali za rufani zilizoko Mwanza, Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, hivyo huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo zitapunguza gharama za kusafiri kutafuta huduma za afya.
"Pamoja na mambo ambayo nimeyasema, niwapongeze kwa kazi kubwa iliyofanyika katika hospitali hii. Nimeona vifaa vya kisasa kabisa vipo hapa ambavyo tulikuwa tumezoea kuviona katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.
"Kwa sasa vifaa hivyo vipo hapa Katavi, hii itasaidia kupunguza gharama za wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya afya," Rais alisema.

Rais Samia pia aliwataka wananchi kujiunga na bima ya afya ili kuwapunguzia gharama za matibabu.
Rais Samia pia alizindua jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi lililogharimu zaidi ya Sh. bilioni 1.4.
Alisema serikali itaendelea kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Kuboresha Mifumo ya Haki Jinai, ikiwamo kuboresha miundombinu ya Jeshi la Polisi na vituo vyake pamoja na utendaji wa watumishi.
Alipongeza jeshi hilo kwa kuendelea kutunza usalama katika Mkoa wa Katavi licha ya kuwa na mwingiliano wa watu kutoka nje ya mkoa huo sambamba na kuimarisha usalama wa kisiasa ndani ya mkoa.
Vilevile, Rais Samia alizindua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vya kuhifadhi nafaka, akielekeza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuwezesha Mkoa wa Katavi kuwa kanda inayojitegemea kwenye ununuzi na uhifadhi wa nafaka.

Sambamba na hiyo, Rais Dk. Samia alizindua msimu mpya wa ununuzi wa nafaka kwa mpaka 2024/25 katika maghala ya NFRA yaliyoko Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi na kutaka wanunuzi kuzingatia haki wakati wa ununuzi na kuwapatia wakulima bei nzuri ya mazao.
Mradi huo utasaidia nchi kuwa na uhakika wa chakula na kupunguza upotevu wa chakula baada ya kuvunwa na utaongeza uhifadhi wa nafaka kwa Mkoa wa Katavi kutoka tani 5,000 hadi 28,000.

Chanzo: Nipashe
Wapeni nafasi watoto wa kike waweze kusoma na kutimiza malengo yao - Rais Samia
Reviewed by Zero Degree
on
7/15/2024 09:27:00 AM
Rating: