Wanusurika kifo nyumba ya kulala wageni ikiungua
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Kagera wamefanikiwa kuzima moto uliounguza nyumba ya kulaza wageni (West End Bar) iliyopo karibu na kituo kikuu cha mabasi Bukoba.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa moto huo wamesema ulianza kuwaka majira ya saa 10 usiku wa kuamkia leo ambapo umeteketeza mali zilizokuwemo.
Miongoni mwa wageni waliokuwa kwenye nyumba hiyo amesema kuwa alikuwa amelala akaanza kusumbuliwa na moshi mkali huku akisikia kelele za wenzake wakiomba msaada na yeye akaamka na kuanza kutafuta njia ya kutoka.
Miongoni mwa wageni waliokuwa kwenye nyumba hiyo amesema kuwa alikuwa amelala akaanza kusumbuliwa na moshi mkali huku akisikia kelele za wenzake wakiomba msaada na yeye akaamka na kuanza kutafuta njia ya kutoka.
Wanusurika kifo nyumba ya kulala wageni ikiungua
Reviewed by Zero Degree
on
7/20/2024 08:20:00 PM
Rating: