Yanga yasafiri kwenda Sauzi pamoja na Baleke
Kikosi cha wachezaji wa Yanga kimeondoka nchini jana mchana kwenda nchini Afrika Kusini kucheza mechi kadhaa za kirafiki pamoja na michuano ya Kombe la Toyota, kikiongozana na straika wa zamani wa Simba, Jean Baleke.
Baleke alionekana jana akiwa pamoja na wachezaji wa Yanga waliokuwa wakisafiri na kikosi hicho, ingawa mwenyewe hakutaka kuonekana.
Alivaa kofia ambayo ilificha karibu asilimia 90 ya sura yake, pamoja na spika za masikioni ikionekana wazi lengo lilikuwa ni kutovutia wanahabari na watu waliofika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, hata hivyo haikuwa kama alivyotarajia.
Badala yake alitambulika kiurahisi na kuwa ndiye kivutio pekee uwanjani hapo, akifuatwa yeye na wanahabari wakimuuliza maswali kadhaa, lakini hakujibu chochote zaidi ya kusonga mbele ili kuungana na wenzake kuingia milango ya uwanjani hapo kabla ya safari kuanza.
Alikuwa amevaa jezi ya njano, kaptura nyeusi na raba nyeupe, akionekana kutembea haraka haraka kukwepa macho ya watu pamoja na wanahabari.

Pamoja na kuwapo tetesi kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa straika huyo wa zamani wa Simba, raia wa Jamhuri ya Kidemikrasi ya Congo, kuwa na mpango wa kujiunga na Yanga, huku vingine vikisema wameshamalizana, lakini hadi leo klabu hiyo haijatangaza lolote kuhusu usajili huo.
Kuonekana kuwa kwenye kundi la wachezaji walioondoka kwenda Sauzi, kunadhihirisha kuwa mchezaji huyo wakati wowote klabu hiyo itamtangaza rasmi kuwa mchezaji wao.
Straika huyo alijiunga na Simba 2023 na aliachwa 2024, akarejea klabu yake ya TP Mazembe inayommiliki, ambao nao walimtoa tena kwa mkopo katika Klabu ya Al Ittihad ya Libya.
Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, amesema kikosi kimeondoka kwa mialiko miwili tofauti.

Alisema kutakuwa na michuano maalum ya Mpumalanga na ile ya Kombe la Toyota ambayo ilihabarishwa siku chache zilizopita.
"Niwaambie tu wanachama na mashabiki wa Yanga, hii siyo 'pre season', sisi kambi yetu ya maandalizi itakuwa pale pale Kigamboni, lakini kilichobadilika ni kwamba wakati huu wa 'pre seasons', kila nchi na klabu zinaanda mashindano maalum ya kujipima nguvu kabla ya mashindano kuanza, hivyo tumepokea ofa nyingi za klabu kutualika.
"Tumekubali mialiko miwili tu, moja ni ya timu ya TS Galaxy ya Mpumalanga ambayo inashiriki Ligi ya Afrika Kusini, pale kuna mashindano ambayo pia tumealikwa na tulishawatangazia ya Kombe la Toyota," alisema.
Kwa mujibu wa Kamwe, Yanga itacheza mechi ya kwanza Juni 20 dhidi ya timu ya Ligi Kuu ya Ujerumani Augsburg, katika mechi maalum ya Mpumalanga, kabla ya kucheza na wenyeji wao TS Galaxy, Julai 24. Alisema baada ya mechi hiyo watakwenda kucheza Kombe la Toyota dhidi ya Kaizer Chiefs Julai 28, kabla ya kugeuza kurudi nchini kuendelea na kambi yao Kigamboni, tayari kwa Wiki ya Mwananchi.

Chanzo: Nipashe
Yanga yasafiri kwenda Sauzi pamoja na Baleke
Reviewed by Zero Degree
on
7/19/2024 07:21:00 AM
Rating: