Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 19 Julai, 2024
Chelsea wameripotiwa kuulizia kupatikana kwa mshambuliaji wa Ureno Goncalo Ramos, mwenye umri wa miaka 23, na mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 25, wa Paris St-Germain ili kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku. (HITC)
Tottenham wanalenga kuipiku Fulham kupata saini ya kiungo wa kati wa Manchester United na Scotland Scott McTominay, 27.
Brentford wanatarajiwa kupunguza gharama ya mshambuliaji wa England Ivan Toney, 28 hadi chini ya pauni milioni 50 baada ya kukosa ofa kutoka kwa klabu nyingine. (Sun)
Arsenal wanatazamia kusitisha nia yao ya kumnunua mlinzi wa Uingereza Marc Guehi huku Crystal Palace wakihitaji zaidi ya pauni milioni 70 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24. (Mirror)
Manchester United bado wanavutiwa na kiungo wa Paris St-Germain kutoka Uruguay Manuel Ugarte, 23. (Sky Sports)
QPR wanavutiwa na winga wa zamani wa Bayern Munich Sarpreet Singh, 25.
Tottenham wamekuwa wakiwasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Canada Jonathan David, 24, kabla ya kuwasilisha ofa kwa Lille. (Football Insider)
Lille imetishia kutomchezesha beki Mfaransa Leny Yoro, 18, katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake ikiwa hatakubali kujiunga na Manchester United. (Marca)
Liverpool wamepunguza nia ya kumnunua Yoro kufuatia masharti yake ya kutaka kuhakikishiwa muda wa kucheza Anfield. (Athletic)
Beki wa Italia Riccardo Calafiori, mwenye umri wa miaka 22, ameombwa kushiriki katika maandalizi ya msimu mpya wa Bologna huku Arsenal ikijaribu kufikia makubaliano juu ya thamani yake. (Evening Standard)
Chelsea wameripotiwa kuwasiliana na klabu ya RC Lens kumsajili mshambuliaji Elye Wahi, 21, baada ya The Blues kushindwa kumpata Mfaransa huyo msimu uliopita. (L'Equipe)
Lyon wanaripotiwa kuwa tayari kutangaza usajili mshambuliaji wa Southampton mwenye umri wa miaka 16 Alejandro Gomes Rodriguez baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 16 kusaini mkataba wa miaka mitatu. (Fabrizio Romano)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 19 Julai, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
7/19/2024 07:40:00 AM
Rating: