Wafanyabiashara hakikisheni mnazingatia sheria ya alama za bidhaa
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanazingatia sheria ya alama za bidhaa ya mwaka 1993, iliyofanyiwa marekebisho inayokataza kuingiza, kuuza na kuhifadhi bidhaa bandia kwani adhabu yake ni kifungo na faini.
Akisoma maagizo manne katika hotuba ya Waziri Mkuu leo Julai 18 ukumbi wa Milimani City jijini Dar es Salaam kwa wadau mbalimbali wa udhibiti bidhaa bandia Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe aliyemuwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Amesema wadau wanatakiwa kuzingatia sheria ya alama na kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC), kudhibiti bidhaa bandia ili kukuza biashara na uwekezaji nchini.
Katika hotuba hiyo ya ufunguzi wa kongamano la kilele cha udhibiti wa bidhaa bandia pia mada mbalimbali za udhibiti wa bidhaa bandia zimejadiliwa.
Akitaja maagizo mengine, amewataka wamiliki wa nembo nchini kuhakikisha wanafuatialia bidhaa zao na kuziwasilisha FCC pale wanapogundua wafanyabiashara wanatumia bidhaa zao zilizobadilishwa uhalisia.
Akitaja maagizo mengine, amewataka wamiliki wa nembo nchini kuhakikisha wanafuatialia bidhaa zao na kuziwasilisha FCC pale wanapogundua wafanyabiashara wanatumia bidhaa zao zilizobadilishwa uhalisia.
“Endeleeni kutoa elimu kwa walaji juu ya athari za bidhaa bandia, ambapo Wakala wa Forodha kwa kushirikiana na FCC hakikisheni bidhaa bandia haziingii kupitia bandari na sehemu za mipakani,” amesema.
Ameitaka FCC kushirikiana na Taasisi zingine kudhibiti bidhaa hizo kuhakikisha wawekezaji wanakuwa na imani, katika ukanda wa Afrika Mashariki (EAC) na ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri Mkuu Majaliwa amesema, udhibiti wa bidhaa bandia sio jambo la mtu mmoja, hivyo washirikiane wote kuhakikisha wanadhibiti suala hilo ambapo kazi hiyo ikifanyika vizuri na kwa mafanikio zaidi itavutia wawekezaji.
Amesisitiza FCC kuongeza wigo wa mashirikiano na mashirika mbalimbali ya kimataifa ya biashara na udhibiti wa bidhaa bandia kuelimisha wadau kuhusu madhara ya bidhaa bandia.
Amesema wamiliki wa bidhaa washirikane na FCC katika kutoa elimu ya alama zao na kushirikiana na mabalozi kuwaelemisha wafanyabishara wa nchi zao juu ya athari za bidhaa bandia.
Wafanyabiashara hakikisheni mnazingatia sheria ya alama za bidhaa
Reviewed by Zero Degree
on
7/19/2024 07:59:00 AM
Rating: