UMEISIKIA HIYOO...? ETI RAISI MUGABE KUMRITHISHA MADARAKA MKEWE MWENYE UMRI WA MIAKA 49.....
Kuzaliwa kwa utawala wa kinasaba sio jambo jepesi kubashiri.
Lakini wananchi wengi wa Zimbabwe kwa sasa wanaonekana kushawishika kuwa kuna uwezekano wa familia ya Mugabe kuingia katika orodha hiyo ya kurithishana madaraka.
Rais Mugabe ana umri wa miaka 90. Mke wake, Grace, ana umri wa miaka 49.
Uvumi wa kurithishana madaraka umekuwa gumzo la kisiasa nchini Zimbabwe kwa miaka mingi, lakini Grace Mugabe katika miaka ya karibuni ameibuka kama mtu ambaye ataweza kumrithi mumuwe madaraka ya uongozi wa nchi ya Zimbabwe.
Watu wa nje wamesikia tabia ya mke wa Rais Mugabe ambaye ni karani muhtasi wake wa zamani kutuhumiwa kufanya manunuzi yasiyo na mpangilio na katika tukio lingine kumpiga ngumi mwandishi wa habari wa Uingereza huko Hong Kong; na kufanya mambo mengine ambayo yanavuka mpaka kama mke wa kiongozi.
Vyombo vya habari vya Zimbabwe, kwa kulinganisha vimedhamiria kumjenga Bi Grace Mugabe kuwa mtu wa kujitolea kwake katika kazi za kijamii.
Wazo la "Rais Grace" kwanza alipata fursa hii mwezi Agosti wakati Bi Mugabe – mwanafunzi katika siasa, bila kutarajiwa aliidhinishwa kama kiongozi mpya wa Umoja wa Wanawake wa chama tawala cha Zanu-PF - jukumu ambalo ni kubwa na litathibitishwa na mkutano mkuu wa chama hicho mwezi Desemba 2014.
Moto ulichochewa mwezi huu wakati mke huyo wa Rais Mugabe alipotunukiwa heshima ya kuwa Dokta Mugabe – Alitunukiwa shahada ya PhD katika sosiolojia miezi miwili baada ya kujiandikisha katika chuo kikuu cha Zimbabwe, na tasnifu yake haipo katika hifadhi ya mtandao wa chuo kikuu hicho.
Uchambuzi wa kina unaonyesha kuwa Bi Mugabe hana nafasi ya kuwa rais, na anatumiwa na kundi moja ndani ya chama cha Zanu-PF.
"Ni rahisi kuelezea. Ameletwa kama njia ya kumzuia Joyce Mujuru kwa njia yoyote ile," anasema mchambuzi mwandamizi wa masuala ya kisiasa Ibbo Mandaza.
Bi Mujuru ni makamu wa rais na anaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kumrithi Rais Mugabe.
"Wakati mume wake akiondoka ndiyo mwisho wake wa kazi ya uanasiasa, kama kweli kuna kazi ya aina hiyo" anasema mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Zimbabwe,anasema Ibbo Mandaza, akitupilia mbali wazo la kuendelea kuwa na utawala wa familia ya Mugabe.
Nadharia nyingine ni kwamba Rais Mugabe anamjenga mke wake ili kuyayumbisha makundi yote ndani ya chama cha Zanu-PF, na kuimarisha nafasi yake ya urais.
Dewa Mavhinga, kutoka Human Rights Watch, anaamini kuwa rais amefanya kosa kubwa kumleta mtu ambaye hana ujuzi wowote wa siasa.
"Inaonyesha kuwa Rais Mugabe hamwaamini mtu yeyote karibu naye"Dewa Mavhinga.
UMEISIKIA HIYOO...? ETI RAISI MUGABE KUMRITHISHA MADARAKA MKEWE MWENYE UMRI WA MIAKA 49.....
Reviewed by Zero Degree
on
9/29/2014 06:36:00 PM
Rating: