Loading...

Taxi zasusia kumbeba msanii mweusi Australia


Msanii nguli raia wa Australia al maarufu ''Uncle'' amekiri kuwa amebaguliwa mara nyingi tu hata na madereva wa teksi wanaokataa kumbeba.

Jack Charles amesema kuwa katika siku tatu zilizopita madereva wa teksi wamesusia kumbeba mara 2 licha ya umaarufu wake kama 'Uncle'
Meneja wake Patrice Capogreco, sasa anasema kuwa msanii huyo anatafakari kuwafungulia mashtaka ya ubaguzi madereva hao wa teksi na kampuni zilizowaajiri.
Tukio la kwanza lilitokea usiku wa Jumatano iliyopita mjini Melbourne msanii huyo Charles alipokuwa akitoka kwenye dhifa aliyotuzwa taji la ''Victorian Senior Australian of the Year''.
Image captionMsanii huyo anatafakari kuwafungulia mashtaka ya ubaguzi
Yamkini alipomsimamisha dereva mmoja wa teksi alidai alipwe kwanza kwani ''alihofia msanii huyo hakuwa na pesa za kulipa''
Na hata kabla hajasahau tukio hilo la kibaguzi, 'uncle' kama anavyofahamika, alisimamisha teksi nyengine impeleke kwenye uwanja wa ndege wa Melbourne ijumaa.
'uncle' aliwachwa ameduwaa dereva mwengine wa taksi alipovurumisha gari lake na kutoweka.
Halmashauri inayosimamia utoaji leseni katika mji huo tayari umeanzisha uchunguzi kuhusiana na matukio hayo.
Msemaji wake ameiambia BBC kuwa halmashauri hiyo haitavumilia ubaguzi wa aina yeyote.
Image captionHalmashauri inayosimamia utoaji leseni katika mji huo tayari umeanzisha uchunguzi kuhusiana na matukio hayo.
Halmashauri hiyo ilionya kuwa ''madereva wa teksi sharti wawe tayari kumhudumia mgeni yeyote bila kumbagua kwa misingi ya rangi ,tabia ama jinsia''
''Nauli ya teksi kuanzia saa nne usiku sharti ilipwe na mteja kabla hajabebwa kuanzia saa nne hadi saa kumi na moja asubuhi.
''Uncle'' ameiambia BBC kuwa sio tukio la ajabu miongoni mwa wa-Australia wa asili.
Mara nyingi wa-Australia wa asili hulazimika kuomba msaada wa wageni kuwasimamishia teksi.

Source: BBC
Taxi zasusia kumbeba msanii mweusi Australia Taxi zasusia kumbeba msanii mweusi Australia Reviewed by Zero Degree on 10/31/2015 07:23:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.