Loading...

Bunge la Tanzania lapata spika mpya


Job Ole Ndugai 
Job Ole Ndugai ndie spika mpya wa bunge la Tanzania. Ndugai mwenye umri wa miaka 55 alijipatia theluthi mbili ya kura zinazohitajika. Alikuwa naibu wa spika wa bunge lililomalizika.

Ndugai anatarajiwa kuliongoza bunge lenye zaidi ya wabunge 100 kutoka upinzani ,ikiwa ndio idadi kubwa zaidi kuwahi kuchaguliwa katika bunge hilo.
Kulikuwa na wagombea 8 waliowania wadhfa huo wa spika,lakini mwishowe ushindani ulikuwa kati ya mgombea wa chama tawala cha CCM Job Ole Ndugai na mwenzake wa upinzani Goodluck Ole Medeye kutoka chama cha Chadema.
Bunge jipya litakuwa na wanachama 394,ikiwa linawawakalishi 30 zaidi ikilinganishwa na bunge lililopita kufuatia kubuniwa kwa maeneo mapya ya ubunge.
Bunge la Tanzania lapata spika mpya Bunge la Tanzania lapata spika mpya Reviewed by Zero Degree on 11/17/2015 04:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.