Loading...

CCM yanyakua viti 64 maalum,Chadema 36

Rais John Pombe Magufuli na aliyekuwa mgombea wa urais kupitia tiketi ya Chadema Edward Lowassa
Chama cha CCM kimenyakua idadi kubwa ya viti vya wabunge maalum miongoni mwa vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita.

CCM kimejipatia viti 64, huku CHADEMA kijipatia viti 36 kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.
Chama cha Upinzani CUF nacho kimejipatia viti 10.
Akizungumza na waandishi wa habari,jaji Damian Lubuva aidha amesema kuwa idadi ya viti maalum vya wabunge wanawake imepanda hadi kufikia 40.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania Damian Lubuva
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ,idadi hiyo imetolewa kwa vyama hivyo baada ya kukidhi vigezo vya katiba na sheria ya kupata asilimia tano ya kura zote halali za ubunge.
Amesema kutokana na uchaguzi huo CCM ilipata kura za ubunge milioni 8,333,953, huku CHADEMA ikipata kura 4,627,923 nayo CUF ikipata kura 1,257,051.
Jaji lubuva amesema kuwa kutokana na majimbo 8 ambayo hayakufanya uchaguzi ,mgawanyo wa viti maalum sasa ni 110 ambapo viti vitatu vilivyosalia vitagawanywa baada ya kufanyika kwa uchaguzi katika majimbo hayo.


CCM yanyakua viti 64 maalum,Chadema 36 CCM yanyakua viti 64 maalum,Chadema 36 Reviewed by Zero Degree on 11/07/2015 04:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.