Loading...

Korti: Wafuasi wa chadema sasa ruksa kumuaga Mawazo


Dar, Mwanza .Mahakama Kuu kanda ya Mwanza leo mchana imetengua amri ya polisi inayokataza waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Alphonce Mawazo.


Polisi ilipiga marufuku uagaji wa mwili wa kiongozi huyo ambaye pia alikuwa mgombea ubunge katika jimbo la Busanda kupitia Chadema kwa sababu ilizodai ni za kiusalama na hofu ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, zuio la polisi mkoani Mwanza halikuwa sahihi. Baada ya kutoa hukumu hiyo, chombo hicho cha kutoa haki kilizitaka pande tatu; Chadema, familia na Jeshi la Polisi Mwanza kukutana haraka iwezekanavyo ili kufanya maandalizi ya kuuaga mwili huo kwa amani na utulivu.



More Comments & shares to this story!!!
Korti: Wafuasi wa chadema sasa ruksa kumuaga Mawazo Korti: Wafuasi wa chadema sasa ruksa kumuaga Mawazo Reviewed by Zero Degree on 11/26/2015 06:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.