Wachina kizimbani kwa pembe za faru
Mbeya. Raia wanne kutoka China, jana walipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya kujibu mashtaka matatu ya uhujumu uchumi likiwamo la kukutwa na pembe kumi na moja za faru zenye thamani ya Sh 902.8milioni.
Washtakiwa hao ni pamoja na Song Leo (33), Xiao Shaodan (29), Chen Jianlin
(34) na Hu Liang (30).
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa akisaidiana na Simon Wankyo,
alidai kuwa washtakiwa wote kwa pamoja walishiriki kuhujumu uchumi kinyume cha
sheria ya nchi.
Pia, alidai kuwa walipanga njama na kutekeleza kuingiza nchini pembe hizo za
faru bila kibali cha Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa, kwa kumiliki
nyara hizo bila kibali.
Mulisa alidai kuwa washtakiwa walikamatwa Novemba 6, mwaka huu katika mpaka
wa Kasumulu wilayani Kyela wakiwa wamezificha pembe hizo kwenye gari walilokuwa
wakisafiria kutoka nchini Malawi kuja Tanzania.
Hata hivyo, washtakiwa wote walikana mashtaka na Wakili Mulisa alisema
upelelezi wa shauri hilo umekamilika.
Alimuomba Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa, Michael Mteite apange tarehe ya
kuendelea kusikilizwa kesi hiyo.
Wakili wa upande wa utetezi, Ladslaus Lwekaza aliiomba mahakama iwapatie
dhamana wateja wake kwa madai kwamba mashtaka wanayokabiliwa nayo yanatoa fursa
ya kuwapo kwa dhamana hiyo. Hoja hiyo ilipingwa na mawakili wa Jamhuri, waliodai
kuwa Mkurugenzi wa mashtaka amezuia dhamana.
Mteite alikubaliana na hoja ya upande wa mashtaka ya kuzuia dhamana kwa
washtakiwa hao na aliamuru warudishwe mahabusu. Kesi hiyo itaendelea leo na
itasikilizwa kwa mfululizo siku mbili.
Source: Mwananchi
Mshirikishe na mwenzako kwa kushare habari hii kadri uwezavyo!!!!
Source: Mwananchi
Mshirikishe na mwenzako kwa kushare habari hii kadri uwezavyo!!!!
Wachina kizimbani kwa pembe za faru
Reviewed by Zero Degree
on
11/25/2015 01:12:00 PM
Rating: