Loading...

Watano wafia mgodini Geita!!


Geita. Wakati ombwe ya wachimbaji wa machimbo ya Nyangalata wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga walikoishi siku 41 kabla ya kuokolewa halijafutika, wachimbaji wadogo watano wamekufa kwa kufukiwa na kifusi katika machimbo ya Mgusu yaliyopo Kijiji cha Mgusu wilayani Geita linalomilikiwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita (GGM).

 
Wachimbaji hao waliingia katika machimbo yaliyopo kijiji cha Mgusu eneo la Prospect 30 kinyemela usiku wa kuamkia jana majira ya 6:30 usiku na kufukiwa na kifusi wakati wakichimba dhahabu.

Shughuli ya kufukua miili hiyo ilifanywa na wachimbaji wadogo kwa kushirikiana na Kampuni hiyo tangu asubuhi hadi saa 10:15 jioni na kuipata mili hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo aliwataja waliokufa kuwa ni Emmanuel Emmanuel, Lucas Deus, Maliatabu Budonyanga, Clement Richard na Baraka Katunzi.





Comment & Share this story!!
Watano wafia mgodini Geita!! Watano wafia mgodini Geita!! Reviewed by Zero Degree on 11/30/2015 03:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.