Loading...

Habari za hivi punde: Kumetokea Ajali mbaya ya basi mkoani Iringa, watu 12 wasadikika kupoteza maisha na 28 kujeruhiwa.



Taswira kutoka eneo la ajali.

WATU 12 wamepoteza maisha huku wengine 28 wakijeruhiwa leo baada ya basi la New Force One kupata ajali eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Dar es Salaam.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha katika ajali hiyo. Wanane ni wanaume na wanne ni wanawake.




Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasiri ambapo basi la kampuni ya New Force One aina ya Youtong lenye namba za usajili T483 CTF likitoka Tunduma kwenda Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye namba T 616 DEF katika kijiji cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa katika barabara kuu ya Iringa – Dar.

Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilula, kilomita 45 kutoka Iringa Mjini.




Credits: Global publishers



Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!
Habari za hivi punde: Kumetokea Ajali mbaya ya basi mkoani Iringa, watu 12 wasadikika kupoteza maisha na 28 kujeruhiwa. Habari za hivi punde: Kumetokea Ajali mbaya ya basi mkoani Iringa,  watu 12 wasadikika kupoteza maisha na 28 kujeruhiwa. Reviewed by Zero Degree on 12/18/2015 10:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.