Loading...

Jose Mourinho atimuliwa kazi Chelsea, Pep Guardiola, Guus Hiddink n.k wapigiwa upatu kumrithi!!!


Jose Mourinho.

Meneja wa Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Jose Mourinho amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kufululiza kwa matokeo mabovu.



The Blues walishinda Ligi Kuu England msimu uliopita lakini msimu huu mambo yamekuwa kinyume, na wapo nafasi moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja kwenye ligi hiyo.

Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatma ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.



Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.

Chelsea walimaliza ligi wakiwa kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 mpaka sasa.




Mechi ya mwisho kwa Mourinho ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi wa ligi hiyo, Leicester City 2-1.

Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi Jose.



Credits: Global publishers



Mshirikishe namwenzako kuhusu habari hii!!
Jose Mourinho atimuliwa kazi Chelsea, Pep Guardiola, Guus Hiddink n.k wapigiwa upatu kumrithi!!! Jose Mourinho atimuliwa kazi Chelsea, Pep Guardiola, Guus Hiddink n.k wapigiwa upatu kumrithi!!! Reviewed by Zero Degree on 12/17/2015 09:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.